Blog

Nigeria washapendeza Qatar, ila hawaendi!

Sambaza....

Timu mbalimbali Duniani kuelekea kombe la Dunia 2022 Qatar wameanza kutambulisha jezi watakazotumia.

Kwa haraka haraka nimeona jezi ya Nigeria ikisifiwa sana ( imebamba ) kama kawaida yao najua wanafanya kazi na kampuni kubwa ya Nike.

Ila huwezi kukwepa kumpongeza designer hajawahi kufeli na hata kuja kufeli nionavyo Mimi.

Tangu nimeanza kuifahamu timu ya Taifa ya Nigeria katika ya miaka 90 hawajawahi kuzingia kwenye pamba (kiwalo ) kibaya.
Sijui kama unamkubuka Top striker Rashid Yekini Baba wa miraba minne kwa mujibu wa watangazaji wa zamani.

Jezi ilikuwa inamkaa na shughuli inafanyika ipasvyo ndiyo maana pamoja na kufariki kitambo kidogo hadi leo hakuna aliyempita kwa magoli kwenye timu ya Super Eagles.

Sipo kutaka kukuambia Yakin alikuwa na umbo gani yeye na wenzake akina Uche Okwochuku maana Wanageria walio wengi ni Magiantism.

Nipo kuisemea Uzalendo wa mchezaji anapoitwa timu yake ya Taifa ( Commitment) yake.

Kutoa kila awezacho kuifanya Taifa kupata ushindi ,Mchezaji wa timu ya Taifa ni Balozi wa nchi ,Balozi wa wengi walionaki nyumban hivyo kuwa na jezi nzuri au mbaya hakuleti maana kama dhamira ya Uzalendo haipo.

Nimetumia Nigeria kama mfano tu hapa walengwa ni Dunia nzima na wale Wachezaji wasio oja thamani ya timu zao za Taifa wao kila kitu ni ‘Club yangu tu’.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.