Sambaza....

Wawakilishi wa Tanzania kunako michuano ya kimataifa Simba na Yanga, wote wanataraji kuanzia nyumbani michezo yao ya mzunguuko wa kwanza mapema mwezi ujao

Yanga sc, iliyopo kunako michuano ya ligi ya vilabu bingwa barani Afrika, itakuwa nyumbani kuwakaribisha Township Rollers ya Botswana mchezo unaotaraji kupigwa kati ya March 7, kunako uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kabla ya kusafiri hadi Gaborone, Botswana kwa mchezo wa marejeano Machi 17

Simba sc, wao watakuwa kibaruani kati Machi 6, wakiikaribisha klabu ya Al Masry ya Misri kunako uwanja wa taifa jijini Dar es salaam huo ukiwa ni mchezo wa kwanza wa kombe la shirikisho barani Afrika, huku ikitaraji kusafiri hadi Cairo Misri kunako uwanja wa Port Said kwa mchezo wa marejeano utakaopigwa Machi 16

Yanga sc, imefikia hatua hiyo baada ya kuiondosha St Louis kwa ushindi wa jumla wa mabao 2-1 ambapo kwenye wa kwanza uliopigwa kunako dimba la taifa iliibuka na ushindi wa bao 1-0, kabla kulazimisha sare ya 1-1 ugenini kunako dimba la Linite mjini Victoria, Shelisheli

Huku Simba sc, wakiiondosha Gendermarie ya Djibouti kwa ushindi wa jumla ya mabao 5-0 ambapo walishinda 4-0 kunako uwanja wa taifa jijini Dar es salaam kabla ya kuchomoza na ushindi wa bao 1-0 ugenini nchini Djibouti

Sambaza....