Mashindano

Champioship kumenoga, JKT wanaitaka Ligi Kuu.

Sambaza....

Ligi ya Championahip zamani Ligi Daraja la kwanza imezidi kunoga huku vilabu vikipambana kutaka kupanda Ligi Kuu ya NBC mwakani.

Tayari vilabu vyote kumi na sita vinavyoshiriki Ligi hiyo vimeshuka dimbani mara kumi kila mmoja, huku kila timu ikipambana kufanya vyema ili kujiweka katika mazingira mazuri yakupanda daraja.

Mpaka sasa JKT Tanzania wanaongoza ligi hiyo huku pia wakiwa na uwiano mzuri wa kupata ushindi katika Ligi hiyo ngumu nchini. JKT walioshuka daraja misimu miwili iloyopita wanaonyesha hawataki kufanya tena makosa kama msimu uliomalizika ambapo walishindwa kupanda daraja baada ya kushindwa kufurukuta mbele ya Tanzania Prisons katika michezo ya Playoffs.

Uwiano wa ushindi kwenye asilimia katika michezo ya Ligi ya Championship, huku JKT Tanzania wakiwa kinara.

Jkt imesheheni nyota kibao waliowahi kucheza Ligi Kuu kama Hassan Kapalata, Seleman Kassim Selembe, Ally Makarani na Maka Edward.

Mpaka sasa JKT wapo kileleni wakiwa na alama 25 wakifwatiwa na Kitayosce wenye alama 23 na Fountane Gate wakiwa na alama 21. Pamba na Mbuni wanafwata wakina katika nafasi za nne na tano.

Sambaza....