Mashindano

Simba yatambulisha mdhamini mpya, yakoga minoti mingine.

Sambaza....

Klabu ya soka ya Simba leo imefanikiwa kuongeza wadhamini wengine kuelekea katika kilele cha siku ya “Simba Day” itakayofanyika katika uwanja wa Benjamin Mkapa August nane mwaka huu.
Mbele ya waandishi wa habari katika makao makuu ya benki ya CRDB Simba wametangaza kushirikiana na benki ya CRDB katika wiki nzima ya Simba Mpaka kufikia kilele chake katika sikukuu ya wakulima nanenane.

Katika udhamini huo CRDB Bank imetoa kiasi cha shilingi milioni ishirini na tano ili kufanikisha shughuli hiyo ya Tamasha la Simba Day.
Akizungumza mbele ya waandishi wa habari Mkurugenzi mkuu wa benki ya CRDB Abdulmajid Nsekela amesema wao kama CRDB wanapenda michezo na ndio sababu iliyowasukuma kushirikia na Simba katika siku yao.

Abdulamajid Nsekela Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB.

“Si tu kuwa mdau wa michezo lakini pia tumeamua kuwekeza kabisa ili kuwawezesha (Simba) katika tamsha lao, huu ni mwanzo tuu na mengine mengi yanakuja.” Abdulmajid Nsekela

Pia mtendaji mkuu wa klabu ya Simba Barbar Gonzales amesema anafurahia kushirikia na benki inayoongoza Tanzania na anatamani siku moja CRDB wawepo katika jezi ya Simba huku pia akisisitiza kuilinda “brand” ya benki hiyo.

Barbar Gonzales Mtendaji mkuu wa Klabu ya Simba

“Tunawashukuru CRDB wa kuwekeza katika “Simba Day”, wenzetu wameona ukubwa wa Simba. Najua huu ni mwanzo tuu naamini siku moja tutawaona katika jezi yetu. Hata kama kampuni haina rangi nyekundu tupo tayari kufanya nao kazi, tutaheshimu “brand” hatuwezi kubadili rangi ya logo yao.” Barbar Gonzales.

Aidha pia Mtendaji mkuu wa klabu ya Simba Barbar Gonzales ameahidi kushiriki katika CRDB Marathon itakayofanyika August 14 mwaka huu ilioandaliwa na benki hiyo kubwa nchini.

Sambaza....