Sambaza....

Mabingwa wa soka Tanzania bara Yanga sc, imeendeleza ubabe wake katika michuano ya kombe la mapinduzi baada ya kuitandika Zimamoto kwa bao 1-0 kwenye wa kundi B uliopigwa usiku huu kunako uwanja wa Amani, mjini Zanzibar

Bao la Yanga limefungwa na kiungo wake wa ushambuliaji Emmanuel Martin kunako dakika ya 60 kwa kichwa akiunganisha vema klosi ya kiungo mshambuliaji Juma Mahadhi

Yanga sasa imefikisha alama 12, baada ya kupata ushindi katika mechi zake nne, ikilingana kwa alama na Singida United inayoongoza kundi hilo la B kwa wastani mzuri wa mabao, huku zenyewe zikitaraji kukutana kesho majira ya 2:15 usiku kwenye mchezo utakaoamua kiongozi wa kundi hilo.

Sambaza....