Blog

Ahmed Rabie, Mchezaji aliyezushiwa kufa, hali yake ipo hivi..

Sambaza....

Ahmed Rabee, kiungo wa Al Jazira ambaye anaendelea kuuguza majeraha ya kichwa baada ya kuumia katika mechi ya kirafiki ya Mchangani, anaendelea vizuri na huenda akarejea uwanjani hivi karibuni.

Hii ni kwa mujibu wa mtandao wa thenational.ae na uchunguzi ambao kandanda.co.tz umefanya katika tovuti ya klabu na vyombo mbalimbali.

Sheikh Mohammed bin Rashid, Makamu wa Rais na mtawala wa Dubai alipomtembelea Rabee hospitalini.

Meneja wa timu hiyo, Ahmed Saeed, alinukuliwa akisema kuwa Rabee anaendelea vizuri na atarudi uwanjani hivi karibuni. Na madaktari wanasema hakupata maumivu mabaya kama walivyodhani hapo kabla. Katika mtandao wa klabu hiyo ripoti yao ya mwisho ni kuwa Rabee anaendelea vizuri na matibabu.

Al Jazira ilikuwa ikicheza na Emirates Club katika mji wa Al Khawaneej huko Dubai. Rabee alipigwa ‘push’ na mchezaji mwenzake na kujigonga kisogo katika bango la tangazo lililo nje ya uwanja huo.

Rabia akiwa kwenye moja ya mechi

Baada ya Sheikh Mohammed kumtembelea Rabie, alitoa angalizo kwa mamlaka za michezo kufuatilia na kuangalia usalama wa viwanja na vituo vyote vya michezo katika UAE.

Meneja Saeed amesema kuwa, kwa taarifa alizozipata kutoka kwa madaktari wa timu, Rabia atakaa nje kwa wiki 5 hadi 6 kisha kurudi tena uwanjani. Meneja huyo pia alimshukuru makamu wa Rais kwa kitendo chake cha kuwatembelea hospitalini na kutoa magizo ya kiusalama kwa mamlaka husika juu ya miundombinu ya viwanja na usalama wake.

Rabie ni mchezaji wa Jazira tangu msimu wa mwaka 2012 na amekuwa akipata nafasi nyingi za kucheza katika klabu hiyo kama kiungo mshambuliaji ,pia aliitumikia Dubai katika kikosi cha U19 pia Rabia ni miongoni mwa wachezaji wanaounda  kikosi cha taifa chini ya miaka  23.

Tujifunze….

Vitu ambavyo vinazunguka uwanja ni bora watu wa usalama wakawa wanapitia mara kwa mara na kurekebisha kupunguza madhara kama haya.

Kwa upande wa Tanzania, uwanja wa Samora mkoani Iringa pia unaweza kuwa hatarishi, kwakuwa mifereji ya pembeni mwa uwanja haijazibwa.

Ikitokea mchezaji akapitiliza hadi nje ya uwanja kwa kasi kubwa bila kuangalia anaweza vunja mguu.

Agizo la makamu wa Rais wa Dubai, Sheik Mohammed ni vyema kama litakuwa agizo kwa dunia nzima ikiwemo Tanzania. Unaweza ukadhani ni kitu kidogo lakini madhara yake ni makubwa sana kwa afya ya mchezaji na hata mashabiki kwa wakati mwingine.

Hivi ni viwanja vingapi nchini Tanzania vinazunguukwa na miti mirefu na hata minara na mashabiki huwa wanapanda kule juu kuangalia mechi kiharamia?

Bila kusahau viwanja vya taasisi mbalimbali nchini, kiukweli miundombinu yake pembezoni mwa uwan ja hasa mifereji ya maji bado ni hatarishi kwa mchezaji.

 

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x