Blog

Aishi Manula kukosekana leo

Sambaza kwa marafiki....

Aishi Manula na David Mwantika kuukosa mchezo wa leo dhidi ya Kenya kutokana na taarifa za majeruhi ambayo Daktari wa timu ataelezea hapo baadae.

Tanzania, Taifa Stars, inacheza mchezo wake wa kwanza leo kutafuta nafasi ya kucheza CHAN, michuano ya wachezaji wanao cheza Ligi za ndani ya nchi. Mchezo uliopita kati ya Kenya na Tanzania ulikuwa katika michuano ya AFCON 2019 huko Misri, ambapo Stars ilifungwa 3-2.

Je ni wakati wa Metacha kukaa golini, au sasa Juma Kaseja anaanza baada ya kitabmbo sana kukosekana katika kikosi hiki? Endelea kufuatilia.

Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.