Blog

Akina Kichuya wajinasua kushuka daraja!

Sambaza....

Klabu ya soka ya Misri anayoichezea Mtanzania Shiza Ramadhani Kichuya imeendelea na harakati zake za kukwepa panga la kushuka daraja katika Ligi kuu ya nchini Misri kwa kupata ushindi mwembamba mapema leo.

ENNPI leo ilikua uwanjani kumenyana na klabu ya Millitary na kufanikiwa kupata ushindi wa bao moja kwa sifuri huku bao la Ennpi likifungwa dakika ya tisa na mshambuliaji wao  Ahmed Sokri.

Kwa ushindi huo sasa klabu ya Ennpi inafikisha alama 26 na kusogea mpaka nafasi ya 14 huku ikiwa imecheza michezo 27 kwenye ligi inayoshirikisha jumla ya timu 18.

Pia katika Ligi hiyo timu nyingine zinazochezewa na Watanzani wameendelea kupishana katika nafasi tofauti kwenye msimamo. Himid Mao akiwa na Petrojet ipo nafasi ya 15 ikiwa na alama 25 huku Ismailia aliyopo Yahya Zaid ikishika nafasi ya 7 ikiwa na alama 35 wakiwa wamecheza michezo 23.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.