Sambaza....

Mchezaji kinda wa Timu ya soka ya Singida United Ally Hamis Ng’anzi anayecheza nafasi ya kati “Middlefield” amefanikiwa kupata timu ya kusakata kabumbu barani Ulaya katika nchi ya Jamhuri ya Czech kwenye klabu ya  ya MFK VySkov inayoshiriki ligi ya Moravian–Silesian Football League sawa na ligi daraja la tatu.

“Hivyo kwa niaba ya uongozi wa klabu, tunamtakia safari njema na mafanikio mema mchezaji wetu huyu tukiamini atafika mbali katika safari yake ya mpira, hivyo tunaamini kuna wachezaji wengine watapata timu siku si nyingi” imesema taarifa ya Mkurugenzi Mtendaji wa klabu Festo Richard Sanga.

Ally Hamis Ng’anzi amepata timu hiyo ikiwa ni jitihada za klabu ya Singida United kuwatafutia wachezaji wakitanzania nafasi ya kucheza soka kwenye timu mbalimbali barani Afrika na hata nje ya Afrika.

“Tunaendelea kusisitiza nidhamu na kujitambua kwa wachezaji kwamba mpira ni ajira, hivyo wajitambue na wacheze kwa malengo” amesema.

Ng’anzi anasafiri usiku wa leo kuelekea pale Czech Republic kwa ajili ya kuanza maisha yake mapya ya soka.

Sambaza....