Sambaza....

Winga wa West Ham United Michail Antonio amesema mapumziko ya kupisha mechi za Kimataifa zilizokuwepo kwenye kalenda ya FIFA yamekuja katika muda sahihi kwa timu ambazo zilikuwa zimeanza vibaya kwenye ligi kuu ya England ikiwemo West Ham.

Wagonga nyundo hao wa jiji la London wameanza vibaya kwa kufungwa michezo yote ya mwanzo ukiwemo na ule ambao walipoteza kwa bao 1-0 dhidi ya Wolverhampton Wanderers.

Antonio amesema Mapumziko hayo yamesaidia kuwapunguzia Pressure ambayo wamekuwa nayo toka kuanza kwa ligi hasa baada ya vichapo hivyo vya mfululizo wakiwa na kocha mpya Manuel Pellegrini.

“Mapumziko haya wakati mwingine yanakuwa kama Baraka, na wakati mwingine ni kama laana, lakini kwetu imekuwa kama Baraka, kwa sababu yametupa nafasi ya kufuta makosa yetu na kuwaza upya baada kuanza vibaya,” Antonio aliuambia mtandao wa klabu.

“Yametupa nafasi ya kufanya kazi nzuri zaidi na kuwa tayari kuanza upya, tumekuwa tukifanyia kazi maeneo mbalimbali ya kiufundi na kujaribu vitu vipya,” amesema.

West Ham ni miongoni mwa klabu ambazo zilifanya usajili mkubwa katika majira ya joto ambapo wamesajili wachezaji 9 lakini mpaka sasa wamefanikiwa kufunga mabao mawili tu toka kuanza kwa ligi na watasafiri hado Goodson Park kucheza na Everton katika mchezo wa ligi Jumapili.

Sambaza....