Mabingwa Afrika

As Vita kucheza na TP Mazembe CAF ?

Sambaza....

Kwa mujibu wa mtandao wa African Sports Updates, umeonesha taarifa ya As Vita kuishitaki Simba Sc ya Tanzania kwa CAF.

Ratiba ya Ligi ya Mabingwa iliyotoka hivi karibuni

As Vita wanadai kuwa Simba Sc walipulizia sumu kwenye vyumba vya kubadilishia nguo kwenye mechi iliyochezwa tarehe 16 mwezi 3 mwaka 2019 kwenye uwanja wa Taifa.

Kwenye mechi hiyo Simba Sc ilishinda kwa jumla ya magoli 2-1, ushindi ambao uliipa uwezo wa kufuzu kwenye hatua ya robo fainali ya ligi ya mabingwa barani Afrika.

 

Wachezaji wa AS Vita wakiwa nje ya vyumba vya kubadilishia nguo katika uwanja wa taifa.

Na taarifa zinadai kuwa tayari uchunguzi wa madai ya As Vita umeshaanza kufanyika. Na kama itabainika kuna ukweli itasubiriwa adhabu sahihi kwa Simba Sc.

Kandanda.co.tz inafuatilia habari hii kwa undani kupata ukweli zaidi, endelea kufuatilia pia tovuti yetu.

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x