Haaland na wachezaji wenzake wa Borussia Dortimund wakishangilia baada ya kufunga goli.
Stori

Bundesiliga is Back!

Sambaza....

Ligi Kuu nchini Ujerumani  maarufu kama Bundasiliga imerejea rasmi leo baada ya kusimamishwa kwa muda mrefu kutokana na janga la corona lililoikumba dunia nzima kwa ujumla.

Urejeo wa Bundesiliga ni kama kiashirio cha nuru mpya miongoni mwa wapenda soka duniani, kutokana na “ku-miss” kandanda kwa muda mrefu.

Haaland na wachezaji wenzake wa Borussia Dortimund wakishangilia baada ya kufunga goli.

 

Baada ya urejeo huo leo zimepigwa game 5 bila ya mashabiki huku Borusia Dortimund wakionekana wapo moto baada ya kumpiga Shalke 04 bao nne kwa sifuri. Tazama matokeo mengine ya michezo ya leo.

Kesho pia kutakua na michezo mingine miwili ambapo miamba ya soka ya nchini Ujerumani Bayern Munchen  watacheza dhidi ya Union Berlin na pia Fc Koln watakua na kazi dhidi ya Meinz!

Kwa urejeo wa Bundesiliga ni kiashirio kipya cha nusu kwa Ligi nyingine barani Ulaya ambazo pia zina mpango wa kumalizia michezo iliyobaki ili ligi iishe na bingwa apatikane uwanjani. Miongoni mwao ni pamoja na EPL Ligi Kuu nchini Uingereza.

Sambaza....