Mabingwa Ulaya

Emery awatahadhalisha wachezaji wake.

Sambaza kwa marafiki....

Kocha wa Arsenal Unai Emery amesema licha ya matokeo ya mabao 3-1 katika mchezo wa kwanza nusu fainali ya Uropa dhidi ya Valencia, lakini bado anauona mchezo wa marudiano kuwa ni 50-50.

Emery amesema ni matokeo mazuri kuyapata wakiwa nyumbani lakini anaamini kuwa mchezo wa mkondo wa pili utakuwa mgumu zaidi kwa anaifahamu Valencia aliyoifundisha kati ya mwaka 2008 na 2012.

“Ni matokeo mazuri hasa tukiwa tumeyapata nyumbani, lakini mchezo wa mkondo wa pili utakuwa mgumu zaidi na pengine ukawa tofauti kabisa, nafikiri kwa timu zote mbili matokeo bado 50-50,”

“Nawapongeza wachezaji na ninajivuniwa, haikuwa rahisi kutulia na kupata matokeo kama yale na timu ngumu kama Valencia, tunataka kunyakuwa ubingwa ili tuingine moja kwa moja kwenye ligi ya mabingwa Ulaya,” Emery amesema.

Katika mchezo uliopigwa usiku wa kuamkia leo Arsenal imefanikiwa kushinda kwa jumla ya mabao 3-1 licha ya Mouctar Diakhaby kufunga mapema kabisa katika kipindi cha kwanza lakini mabao ya Elexandre Lacaztte na Pierre-Emerick Aubameyang kuifungia Arsenal mabao ya ushindi.

Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.