Blog

Eto’o kumjengea nyumba nahodha wa zamani wa Cameroon.

Sambaza....

Imeripotiwa kwamba Mshambualiaji wa Zamani wa Barcelona na Inter Milan Samuel Eto’o amemuahidi kumnunulia Nyumba nahodha wa zamani wa Timu ya Taifa ya Cameroon Norbert Owona.

Eto’o amefikia maamuzi hayo baada ya Nyota huyo aliyewika na Cameroon katika miaka ya 1960 na 1970 kuripotiwa kwamba hana pa kuishi akiwa na umri wa miaka 67, anaishi kwenye mitaa ya mji wa Douala.

Hivi karibuni Owona alilazwa hospitalini kutokana na Kuugua ugonjwa wa hernia na Eto’o alipomtembelea ndipo akamuahidi kumnunulia nyumba nyote Huyo.

Mbali na hilo pia Eto’o amechanga zaidi ya shilingi Milioni 1.7 kwa ajili ya matibabu ya nahodha huyo katika Mchango maalumu unaoendeshwa na nyota mwingine wa Zamani wa Cameroon Joseph Kamga.

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x