
Klabu ya Everton imethibitisha kuwa itacheza na Mabingwa wa Kenya, Gor Mahia katika mchezo wa kirafiki Novemba 6 mwaka huu katika uwanja wa Goodson Park mjini Liverpool, England.
Everton wamethibitisha tarehe hiyo kwenye Mtandao wao wa Twitter.
Gor Mahia walipata nafasi ya kucheza na Everton baada ya kuwafunga Simba ya Tanzania kwa mabao 2-0 katika mchezo wa fainali ya SportPesa Super Cup uliofanyika mwezi Juni mwaka huu katika uwanja wa Afraha nchini Kenya.
Mwaka jana Eveton walikuja Tanzania mwezi Julai kucheza na Gor Mahia ambapo walifanikiwa kushinda kwa mabao 2-1 katika mchezo ambao ulifanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Unaweza soma hizi pia..
Waandishi wa habari za michezo waigalagaza Unitalent.
Unitalent hawakuishia tuu kufungwa mabao mawili lakini pia waliteseka uwanjani haswa katika eneo la kiungo
Kwanini Boban Hakuyapenda Maisha Ya Ulaya…?
Yumkini Haruna Moshi alishawishiwa kutokukipenda ambacho kingemsaidia maishani. Soma stori hii
Manara: Tunataka kuujaza uwanja Jumamosi!
Msemaji huyo pia ameonyesha ni kwa kiasi gani wamedhamiria kuujaza uwanja huku akitangaza neema kwa mashabiki wa Yanga wataokata tiketi kwenda uwanjani.
Hivi ndivyo tulivyomuua Samatta wetu.
Mimi siyo mpenzi wa mpira wa miguu ila nilisikia Rafiki zake wakimwiita Ronaldinho Gaucho,