Sambaza....

Chama cha soka England kimemkuta na hatia Meneja wa klabu ya Derby County Frank Lampard kwa kosa la kumbwatukia mwamuzi katika mchezo wa ligi ya washindi (England Championship) dhidi ya timu yake na Rotherham United.

Lampard pamoja na Mchezaji wake Tom Lawrence walitolewa nje kwa kadi nyekundu katika mchezo huo wa siku ya Jumamosi ambao ulishuhudia Derby wakifungwa kwa bao 1-0 na kuvunja rekodi ya kushinda mfululizo kwenye ligi hiyo.

Tom Lawrence alitolewa katika dakika ya 58 kwa kumchezea rafu mbaya Richard Towell na dakika tano baadae Rotham United wakapa bao kupitia kwa Ryan Manning kwa njia ya penati baada ya Kyle Vessell kufanyia madhambi ndani ya 18.

Baada ya matukio hayo Lampard alionekana kutotulia katika kiti chake hasa katika dakika ya 77 alipokwenda kumbwatukia mwamuzi kwa vitendo alivyoona kuwa kama timu yake inaonewa, kitendo ambacho kilimfanya mwamuzi wa mchezo huo kumtoa nje kwa kadi nyekundu.

Chama cha soka England kilifungua mashtaka na wanasubiri hadi Alhamis kutoa hukumu, kwani wamempa Lampard hadi muda huo kukata rufaa kama ataona ameonewa.

Sambaza....