Kombe la Dunia

‘Fyeka Burundi’ wanadhani ni maneno tu!

Sambaza....

Timu ya Taifa ya Tanzania leo itaanza safari yake ya kutafuta tiketi ya kucheza fainli za kombe la Dunia Qartar 2022, ikianza na timu ya taifa ya Burundi ugenini. Wadau wa soka nchini wamekuja na kauli mbiu ‘Fyeka Burundi’ ikiwa na maan wanahitaji kusonga na Burundi wanatakiwa kupisha nji.

Jana wakati wa mkutano wa waandishi wa habari, nahodha wa Burundi, Gael Bigirimana, alipuuzia kuli mbiu hiyo akisema ‘ni maneno tu, tukutane uwanjani’ ikikaziwa pia na kocha wa timu hiyo.

Lakini kwa upande wa Tanzania, benchi la ufundi limejiandaa kimchezo na mashabiki pia wamejiandaa nje ya uwanja. Kwahiyo kwa namna fulani kauli mbiu imeeleweka Burundi pia. “Tumedhamiria kufanya vizuri tunaposema kufyeka tumejipanga kusonga hatua inayofuata” Msemaji wa TFF, Cliford Mario Ndimbo alipoongea na mtandao huu.

“Mchezo utakuwa mgumu sababu ya wachezaji kufahamiana kati ya Burundi na Tanzania, lakini tunataka matokeo” Juma Kaseja, golikipa wa Taifa Stars alipokuwa kiongele kuhusu mchezo huo, maneno ambayo hata kocha wa Burundi, Olivier ametoa kama angalizo upande wake.

Tanzania kwa sasa haina ubishi ipo katika sehemu ya juu kabisa kimafanikio katika upande wa Soka, kauli hizi ni sehemu tu ya kuremba na kupendezesh hilo, lakini kuna juhudi kubwa zinafanywa kusonga mbele.

”Mwamba Ngozi huvutia kwake ,kuna kitu cha kukifuatilia soka la Tanzania kwa sasa lipo kwenye upepo wa mafanikio ya pamoja kama nchi” Tigana Lukinja, mtangazaji na mchambuzi wa EATV aliuambia mtandao huu. Tigana yupo pamoja na jopo la waandishi wa habari waliosafiri hadi Burundi kwa Basi.

Tanzania itacheza leo dhidi ya Burundi na kauli mbiu hii kama imeshapuuziwa na Burundi, basi ilete maana sasa ndani ya uwanja zaidi.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.