Miguel Gamondi
Stori

Gamondi na Falsafa Mpya Yanga.

Sambaza....

Falsafa ni imani ya mtu katika kufanya jambo. Mara nyingi watu hufanya mambo kadiri imani zao zinavyowaongoza. Kuwepo kwa utofauti wa kifalsafa baina ya watu ndio imeleta walau maana ndogo ya maisha. Hebu fikiri maisha bila falsafa yangekuwaje.

Pale Yanga kuna Muargentina Miguel Gamondi, huyu ni kocha mkuu wa Yanga alitambulishwa baada ya Yanga kuachana na kocha wake Naserdine Nabi aliyetimkia Far Rabat ya Morrocco.

 

Wakati Yanga ikiwa chini ya Nabi walicheza soka safi wakiwa na falsafa ya tikitaka ambayo walikaba kwa nguvu kiasi na mara nyingi walicheza soka la kasi kiasi, lakini chini ya Mtaalamu Gamondi mambo yamebadilika, jamaa amekuja na falsafa mpya ambapo timu nzima huhusika katika suala la kukaba na kushambulia sio kukaba tu bali kukaba kwa nguvu sana (Gen gen presing), na zoezi hilo hufanyika katika ukanda wa mpinzani ambapo ni rahisi kufika langoni mwa mpinzani na kumwadhibu vikali.

Falsafa hii ilianza kuonekana katika mchezo wa wiki ya Mwananchi dhidi ya Kaizer Chiefs, kisha katika michezo ya Ngao ya jamii pale Tanga ingawa haikuwa kwa kiasi kikubwa.

Mchezo kati ya Yanga na KMC uliopingwa katika uwanja wa Azam Complex pale Chamazi juzi tarehe 23 mwezi huu ulidhihirisha ujio wa falsafa hii ambapo falsafa hii ilijionyesha vema, katika mchezo huu Yanga iliibuka na ushindi wa magoli matano kwa bila.

Dickson Job na Mudathir Yahya wakishangalia bao katika mchezo dhidi ya KMC.

Katika mchezo huu timu nzima ya Yanga ilihusika katika kukaba na kushambulia kwa nguvu kila mchezaji alitimiza jukumu la kukaba kwa nguvu na kutumia makosa ya wapinzani kuwaadhibu ipasavyo.

Falsafa ya kukaba kwa nguvu ina faida na hasara zake, moja ya faida za kukaba kwa nguvu ni kama vile kulazimisha adui kukosea na kumwadhibu. Kukaba kwa nguvu tena katika ukanda wa mpinzani kunafanya zoezi la kushambulia liwe jepesi kwani timu inakuwa karibu na lango la mpinzani na inakuwa ni rahisi kufunga magoli mengi. Mfano mchezo wa Yanga dhidi ya KMC unadhihirisha hili kiasi cha kufunga magoli matano,

Pili, Kuutawala mchezo; Falsafa ya kukaba kwa nguvu mpira unapokuwa kwa mpinzani inasaidia kurudisha umiliki wa mpira na kutawala mchezo.

Khalid Aucho akimdhibiti mchezaji wa KMC.

Changamoto ya Falsafa ni ikiwa timu haina wachezaji sahihi hususani wanaotumia nguvu na wenye kasi kubwa, kwa pale Yanga haiwezi kuwa tatizo kwani wako na kikosi kipana lakini wako na wachezaji wengi vijana na wenye kasi ambao wanaweza kutumika kwa kasi na nguvu ile ile katika muda wote wa mchezo.

Hofu yangu ni moja. Kutokana na falsafa hii ya kukaba kwa nguvu (Gen gen pressing) basi tutarajie rundo la wachezaji kupata majeraha. Falsafa hii ya kukaba kwa nguvu inawataka wachezaji kujitoa kwa zaidi ya 100%, matumizi makubwa ya nguvu kutawafanya wachezaji kupata fatiki na uchovu kupitiliza na kuwafanya iwe rahisi kupata majeraha.

Mfano, Liverpool wanatumia falsafa ya kukaba kwa nguvu nyingi sana na msimu uliopita waliandamwa na majeraha sababu wachezaji walitumika kwa kiasi kikubwa.

Yao akipiga pasi mbele ya Chambo wa KMC.

Sasa nini kifanyike ili falsafa hii iote na kumea vema? Tutawanusuru vipi wachezaji dhidi ya majeraha kutokana na falsafa hii? Jibu ni jepesi mno.

WWW.KANDANDA.CO.TZ iko hapa kujibu na kukutoa mashaka yote uliyonayo, kikubwa endelea kuwa nasi na usisahau kutufuata katika kurasa zetu za kijamii;

Kuajiri wataalamu wa viuongo na tiba ( football scientists); Ipo haja ya Yanga kufanya kazi kwa maelekezo ya wataalamu wa sayansi ya mpira hususani wataalamu wa lishe na tiba pamoja na viuongo, wataalamu hawa watashauri ni vyakula gani wachezaji watapaswa kuvitumia ili kuwaimarisha na vipi vya kuacha kulingana na falsafa hii.

Benchi la ufundi la Yanga!

Lakini pia wataalamu wa viungo na tiba watashauri matumizi ya mchezaji kulingana na hali yake ya kiafya, kwa kufanya hivi itasaidia kulinda afya na viwango vya wachezaji.

NB: USIPIGANE UKANG’ATA SI BORA UKIMBIE.

Sambaza....