Mohamed Hussein "Tshabalala"
Blog

Haji Manara kawakosea adabu wachezaji wa Simba

Sambaza....

Mwandishi wa makala hii anaanza kwa kutoa angalizo hizi ‘Hii ni kwa wenye Akili!!! Haiwahusu mbumbumbu.’ Endelea kuisoma…..


Sikubaliani na kitendo cha Manara cha kuwatupia Lawama wachezaji wa simba. Kwanza kuona kuwa ni rahisi kuwafunga Yanga ni kumkosea Adabu mpinzani wako. Timu zote zlilizopo ligi kuu zinaweza kuifunga Simba as Long as Zipo level moja na ligi Moja. Liverpool na ubora wake wa sasa wanaweza kufungwa na timu yoyote ya EPL. Itategemea na game plan na ubora wa wachezaji katika Siku ya game yenyewe.

Manara anataka wachezaji wa Simba wapambane. Nitamwambia mambo machache sana anayokosea.

1. Kagere, Kanda, Mkude, Manula, na baadhi ya wachezaji wengine walioanza Jana pale Simba umri wao umeshafikia kikomo cha kupambana. Kisaikolojia hawana tena cha kupata kwenye Soka yaani hakuna timu inayoweza kuvutiwa na Kagera au wenye umri wa kulingana naye pale Simba hata kama angelifanya maajabu gani kwenye soka. Hawa kina mkude wamefikia mafanikio ya juu kabisa kwenye soka lake. MTU kama Samata pale alipo ana intrinsic Motivation kuwa nikifanya vizuri nitajiuza zaidi kwenye ligi kubwa zaidi. Kwenye akili ya kina Kagere hakuna hicho kitu. Pili mwili unakataa, uwezo wa akili nao unagoma Manara anataka wapambaneje?

Mzamiru Yasin akimdhibiti Haruna Niyonzima

2. Kauli yake angelitakiwa aiongelee kwenye vikao vya ndani. Sio kila kitu ni cha kuweka kwenye media, kauli yake inawadhalilisha sana wachezaji wa simba. Mimi nikiwahi kufanikiwa kusoma saikolojia kidogo, tunapofundisha darasani ukimwambia mwanafunzi huwezi hatokaa aweze kweli umemuua kabisa. Manara anadai kuna wachezaji hawastahili kuvaa Jersey ya Simba. Anayesema haya dirisha dogo likiwa linaelekea kufungwa na mzunguko wa pili haujaanza, hivi hawa wachezaji wanajisikiaje? What if wakianza kugoma kucheza kwa kujituma? Wachezaji kibao wamewahi kucheza chini ya kiwango kutokana na kauli ya viongozi. Manara angelitakiwa awapongeze kwanza wachezaji kuna waliondoka pale wameumia kabisa wakiipigania timu, mpira huwa unakataa kabisa na kukupa matokeo ya ajabu na ambayo hukutarajia. Hata kama ni kuwasema angelitakiwa awaseme kwenye kambi kimya kimya.

3. Manara ni Nani pale Simba? Mipaka ya Nazi yake ni ipi? Toka nimeanza kufuatilia Moira sijawahi kuona msemaji wa timu akiongelea mambo technical ya timu, akichambua kukosea kwa wachezaji hiyo ni kazi ya Kocha. Manara anasema kama nani? Huu mdomo wa manara hauwezi kufungwa na kupangiwa vya kuongea?

4. Manara yupo very Emotional huwezi kuamini kama ni msemaji wa club kubwa kama Simba. Manara anagombana na kila MTU, waandishi, wasemaji wenzeke, wachezaji wake nk. Hii idara ya usemaji ni professional kabisa, Sijui kama Manara kasomea au lah ila huwa anakosea sana.

Manara kawakosea sana Wachezaji awaombe msamaha.

Anamaliza kwa kusema ‘Wenye akili wamenielewa’


Thadei Ole Mushi.
0712702602


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.