Sambaza....

Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Liverpool Adam Lallana huenda akarejea uwanjani kuendelea na mapambano ya soka baada ya mwezi mmoja, kutokana na jeraha la nyonga alilolipata na kumsababishia kuondolewa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya England kinachojiandaa na mchezo wa ligi ya mataifa ya Ulaya (UEFA Nations League) dhidi ya Hispania na Uswiz.

Jopo la madaktari wa Liverpool limemfanyina vipimo kiungo huyo baada ya kurejea jijini Liverpool, na imebainika jeraha linalomkabili Lallana sio kubwa sana.

Majibu ya vipimo hivyo yamedhihirisha Lallana hatokua nje kwa muda mrefu, na katiki kipindi cha majuma mawili hadi matatu atakua katika hali ya utulivu kabla ya kuanza tena mazoezi.

“Ni tatizo dogo ambalo wamelibaini, nitakua nje uwanja kwa muda wa mwezi mmoja,” alisema Lallana alipohojiwa na Sky Sports.

“Imenisikitisha kukosa sehemu ya michezo ya klabu yangu kwa kipindi cha mwezi mmoja, lakini sina budi kujiuguza na ninaamini nitakaporejea nitakua na ari kubwa ya kushirikiana na wenzangu.

“Bado nina nafasi nyingine ya kuwa miongoni mwa wachezaji watakaoitwa kwenye kikosi cha England, nilipanga kupambana kwa moyo wangu wote katika michuano hii ya UEFA Nations League, lakini ninaamini waliosalia kikosini wana uwezo mkubwa, watafanikisha suala la ushindi.”

Sambaza....