Blog

Inawezekana MO alikuwa anacheza na akili za Wana SIMBA?

Sambaza....

‘MO’ hakuwa na dhamira ya kujiuzulu nafasi yake ya uenyekiti wa bodi ya wakurugenzi baada ya kipigo cha Mtibwa isipokuwa alitaka kupoteza akili za mashabiki kindakindaki wa Simba wanaoamini SIMBA NI KUBWA na haipaswi kufungwa na Mtibwa?

MO anajua akili za mashabiki wa Simba. Anawamudu. Anajua udhaifu wao. Sio wavumilivu. Hawana subira. Hawana huo uvumilivu. Na matokeo yakiendelea kuwa mabaya wanaweza kuacha kabisa kujaza uwanja. Nini afanye wasijadili matokeo na wajadili ufadhili wake?

MO anajua kabisa mashabiki wa Simba wanataka matokeo mazuri. Wapo tayari kuvunja hata viti vya uwanja wa Taifa wakifungwa. Mashabiki wa Simba hawakubali kwamba wa naweza kufungwa na Mwadui au Mtibwa. Hawataki kuamini Yanga anasawazisha goli mbili ndani ya dakika tano.

MANARA na MO wamefanikiwa kuwaaminisha wana SIMBA karibu wote nchi nzima kwamba SIMBA ni kubwa Afrika kuliko hata TP Mazembe. Wanasimba wameamini. Amewahi kusema ‘level zao ni Fc Barcelona’. Unawaeleza nini wakifungwa na Mtibwa? Watoe sare na Yanga?

Mashabiki wa Simba wanaimba jina la “UCHEBE” uwanjani. Kocha aliyewapeleka kwenye makundi ya ligi ya mabingwa Africa. Hawataki kusikia jina la “SVEN” na wanasema wameletewa ‘Vladimir Putin aliyepooza’ sasa unawaambia nini wamsahau UCHEBE?

Hakuna namna. Tengeneza tukio. Tangaza kujiuzulu. Wagusie kuhusu ulipaji mishahara. Waache wajadili kwa muda. Tangaza kurejea baada ya saa 24. Na mjadala utakuwa “MO” na sio SVEN au matokeo ya Simba vs Mtibwa kukosa MAPINDUZI cup. Akili ni nyingi.

Bilioni 4 za kitanzania ni kitu gani kwa MO ambaye anatangaza bidhaa zake kwenye fulana za Simba, kwa mkataba usiojulikana hadharani kwa mashabiki wa Simba!? Hawezi kujiondoa Simba kizembe hivyo kisa kufungwa na Mtibwa..

Tweet ya Jana jioni baada ya kupoteza fainali.

SIMBA kafungwa na Al Ahly goli tano, Simba kachezea goli tano nyingine kwa AS Vita, jumla goli KUMI. Simba akachezea goli tatu kutoka kwa JS Saoura. Jumla ngapi? 13. Lakini hakujiuzulu, ajiuzulu kufungwa na Mtibwa kwenye mashindano ya MILIONI 15?

MWAMEDI kafanikiwa kwa 100%. Hajang’atuka. Bado yupo ndani ya Simba kama mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa Simba. Bado anaendelea kuitumia Simba. Amewaunganisha wanasimba. Sasa wanajadili jina lake na sio matokeo ya Simba huko Zanzibar.

Mashabiki wa Simba wao wanataka kuona timu ikishinda. Hawana shida ya kuuliza wapi zilipo 20 alizonunua hiyo Simba. Zinafanya kazi gani? Hawana muda wa kuuliza haya kama wakimfunga MBAO fc na KMC kwenye ligi kuu. Kweli tena. MO anajua hili..

Wapi zilipo $600,000 za, CAF kwa kuvuka makundi ligi ya mabingwa Afrika? Shabiki wa Simba anapata wapi akili ya kuhoji hayo endapo wanamfunga Polisi Tanzania na Kagera Sugar? Au kwenda Tanga na kumfunga Coastal Union?

Mo Dewji wakati wa mechi ya kirafiki kati ya Simba SC na Sevilla FC

Kwamba shabiki akaulize gate collection za michezo ya Simba ya ligi ya mabingwa Afrika? Bilioni 5 za Sport pesa? Wapi fedha za MO ENERGY au ni bure? Haki za matangazo AzamTV? Simba TV? TV rights? Shabiki atahoji haya baada ya kumfunga LIPULI?

Akili nyingi za MWAMEDI. Ni mfanyabiashara. Anajua hawezi kuacha Simba kirahisi. Kuna Faida kuendelea kuwepo Simba kwa jina la “shabiki mwekezaji wa Simba” .. Agenda setting! Waswahili wanajadili Tweet zake mbili na sio tena MTIBWA SUGAR kumfunga Simba FAINALI!

Kwanini mwenyekiti wa SIMBA wakati fulani, Ismail Adem Rage alisema mashabiki wengi wa SIMBA ni “_______?”

Vyote vinaweza visiwe sahihi… Hii ni “vipi kama?”


Martine Maranja Masese

Sambaza....