Sambaza....

Ligi Kuu Bara imeendelea tena leo kwa michezo miwili, ambapo Jkt Tanzania wakicheza na Mtibwa Sugar huku Azam wao wakiikaribisha Biashara United sa moja usiku. Katika dimba la Generali Isamuhyo Mbweni jijini Dar es salaam Jkt Tanzania imewakaribisha wakata miwa Mtibwa Sugar ya Morogoro.

Katika mchezo huo Jkt Tanzania imeshindwa kutumia vyema uwanja wao wa nyumbani baada ya kulazimishwa suluhu ya bila kufungana na Mtibwa Sugar huku mchezo ukitawaliwa na ubabe wa hali ya juu kwa wachezaji kuchezea faulo mara nyingi.

Kwa matokeo hayo sasa yanaifanya Jkt Tanzania kufikisha alama 20 wakishuka dimbani mara 24 huku wakiwa nafasi ya 12. Mtibwa Sukari wao wanasogea kutoka nafasi ya 10 mpaka nafasi ya 7 wakiwa na alama 28 wakishuka dimbani mara 20.

Tazama hapa picha za matukio katika mchezo wa leo:

Ismail Mhesa vs Kilemile.
Stamil Mbonde akimtoka mlinzi wa Jkt Tanzania.
Riphat Khamis
Shabani Kado.
Nahodha Shabani Nditti.

Sambaza....