Blog

Kinachomkuta Eboue wacha kimkute tu!

Sambaza....

Kwanza nianze kwa kumshukuru Mungu mwingi wa rehma .

Pili niwe mkweli sijawahi pata kuwa mwandishi kwa namna yoyote ile hivyo muniwie radhi kwa mapungufu yoyote ya kiuandishi .

Kilichonisukuma kuandika ni kuhusu mchezaji mahiri wa soka mwenye mafanikio makubwa ndani na nje ya uwanja, Emmanuel Eboue.

Taarifa zinaeleza, hivi karibuni Emmanuel Eboue amekutwa na matatizo ambayo yamepelekea kukombwa kila kitu na aliyekuwa mkewe bi Aurelie Bertrand ambaye ni raia wa Ubelgiji. Kutokana na tukio hilo, Emmanuel Eboue ambae ni raia wa Ivory Cost, inasemwa anaishi kwa dhiki ,mpaka kufikia kulala kwenye vibaraza vya nyumba za marafiki.

Image result for Emmanuel eboue

Kama binaadamu, nilipousikia mkasa wa mchezaji huyu, nilihuzunika sana,ila mwishoni mwa huzuni natamka wazi kabisa, Kwa hili linalomkuta Emmanuel Eboue wacha limkute na liwakute wote wenye tabia kama yake, Mfa kiranga haliliwi.

Nimesoma maandiko mengi yanayozungumzia uhodari na uwezo Mkubwa wa Emmanuel Eboue pindi akiwa uwanjani na kuelezea fedha nyingi alizokuwa akivuna kwa kazi ya miguu yake aliyojaaliwa na muumba wake na kuziwekeza kwa mke na watoto pekee ,
Kwa kweli sijawahi pata soma popote pale kwa mujibu wa waandishi kinachoonesha mchezaji huyu mahiri nini alifanya kwa wazazi, ndugu, ukoo, wa Ivory cost ,wa afrika na walimwengu kwa ujumla,
Kwa imani yangu kwa kuwa hayakuandikwa naamini hakufanya kabisa maana waandishi katika kipindi hiki kigumu kwa Eboue wameweza kumbuka Chenga alizopiga uwanjani pindi alipokuwa kwenye ubora wake hivyo ni vigumu kutokukumbuka mema na mazuri aliyofanya kwa wazazi, ndugu, ukoo, wa Afrika na walimwengu

Niseme tena huyu Emmanuel Eboue wacha yamkute hayo na mengine na wale wote wenye tabia kama yake, Mfa kiranga haliliwi.

Watu wengi ni wabinafsi na wanafikiri wamezaliwa ili waanzishe familia au wanaweza kufanya lolote kwa Kuwa wao ni wao na wanahiyari yakufanya lolote, huo ni ujinga na upumbavu mkumbwa.
Mwanadamu hayupo huru kufanya lolote, lazima ujue haki za watu kwenye maisha yako na usipozitambua haki hizo ujue unafanya dhulma kubwa dhidi ya hao wenye haki na lazima itakugharimu kwenye maisha yako siku zote.
Mwanadamu hakuzaliwa kuja kuanzisha familia, mwanadamu amezaliwa kuja kuendeleza familia, wapo waliotangulia, wapo waliokufanya Ufike ulipo, na kumbuka Mke na watoto wana haki kubwa sana kwako lakini ni watu waliokukuta ukubwani na pengine ushatajirika.

Image result for emmanuel eboue galatasaray

Narudia, yawezekana watoto na mke /wake wanahaki zao kubwa kuliko wote, lakini isipelekee kudhulumu haki za wengine kwa kisingizio cha watoto na mke / wake zako.

Hakika dunia ni ngumu na zimwi likujualo haliwezi kula likakumaliza na hata likikumaliza ujue kuna namna na hata kuku huamua kula mayai yake inapobidi, pia nimewahi pata sikia mbwa, paka na hata nguruwe hula watoto wanao wazaa wenyewe ila siamini kama wanafanya kwa roho mbaya naamini ipo sababu iliyowafikisha walipofika,
Watu wengi huwatumia ndugu, rafiki na hata wazazi kama vyombo either vya kutunza wanavyovichuma ama kuchuma na kuwapa ujira ili waweze kuishi kwa wakati anamtumikisha na si kuwajengea uwezo ili wajitegemee ili wawe kama wao au zaid ya wao.

Kwa kweli watu wengi hasa kwenye nchi zetu za kiafrika hukwazika sana na kitendo cha kuvukwa/kupitwa kwa namna yoyote ile na aliyemtangulia ,matokeo yake huwatumia ili wao wafanikiwe au kuwaacha kabisa,
Wengi atuna hamu ya kuwa chanzo cha mafanikio ya watu na ikitokea kufanikiwa kwanamna yoyote vile hukwazika. na ndio maana miongoni mwao huwa na falsafa ya chukua chako mapema na akiona ngumu hufikia hata kukudhuru ili awe kama wewe au zaidi, na niwe mkweli iwapo tutakuwa na hamu ya kuwafanya tuliowatangulia eidha kielimu, kiumri, kiuchumi nk ,wawe kama wewe au zaidi ni wazi kabisa hawatafikiri kukufanyia baya kwa namna yoyote ile na hata kama ataamua kufanya baya kwako wapo wengi watakao kukinga na shari hiyo kwa kuwa uliwakinga na mengi na ulijitoa ili wawe walipo na kubwa kuliko yote hupata fadhila nyingi kwa muumba wako.
Haiwi kosa kwa yoyote yule kuamini mke na watoto ni watu ambao upo karibu nao na utakuwa nao karibu kwa vipindi vyote, kosa ni lile unapoamini kuwa uwekezaji wote ni vyema na busara kufanya kwa mke /wake na watoto pekee.

Tunasahau Mke/wake na watoto tumekutana ukubwani .

Ebu tujiulize swali ,hivi wake zetu wanatujua au ni watu wa karibu tu kwa Muda fulani? ?,hivi kuwa karibu na mtu kwa miaka fulani ndio kumjua? ??
Anakujua ulipotokea? , hakika hawezi kukujua mtu kwa kukukuta ukubwani!, ingawaje unaweza kufanikiwa kwa msaada au kushirikiana na watu uliokutana nao ukubwani .

Image result for emmanuel eboue wife photos
kila mafanikio Yana chanzo na lazima tuwe na heshima pamoja na unyenyekevu dhidi ya vyanzo vyetu
Umasikini ukiwa kichwani ni tatizo kuliko ule wa mfukoni, wengi wetu hufikiri juu ya watoto na wake zetu na hudhani uwekezaji ni ule wa ujenzi wa majumba makubwa, tena kwa sisi wa Afrika tunaona ni busara na heshima kubwa kuwa na jumba London na kusahau Abidjan au Dodoma !,
Hivi nani alishakuwa nani kwa ajili ya Eboue tena kwa makusudi yake na sio kwa bahati mbaya, leo imedhihiri kuwa vya ulaya ni vya wazungu na Mfa kiranga haliliwi

Wacha yamkute Emmanuel Eboue na wote wenye tabia kama zake

Cheed Selungwi
03/01/2018

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x