Ligi Kuu

KMC chombo kimepata moto?

Sambaza....

KMC hawakuanza vyema kwenye msimu wa ligi ilionekana kuwa juu yao na baadhi ya watu wakawazungumza kwenye kushuka daraja kutokana na mwenendo wa matokeo yao mabaya.

Mabadiliko ya mara kwa mara kwenye benchi la ufundi nako kulifanya timu isiwe na utulivu kwenye muundo wa kucheza ( pattern) pamoja na ukweli kuna wachezaji wenye vipaji vya juu ( quality) zao zipo juu ila kuna eneo halikutimiza wajibu wake ipasavyo.

Hichi kinachoonekana sasa ni utulivu wa benchi la ufundi” kubeua” mbinu bora na wachezaji kuwa na usikivu na upokevu mzuri ilihali sasa timu inaonekana kupata utulivu na kucheza kiufundi na kimbinu zaidi kitu ambacho tunakitathimini ni kuimarika kwa timu.

Kabla hatujaenda kwenye mapumziko kupisha maradhi ya Corona timu ilicheza michezo mitano ya Ligi Kuu na kushinda minne huku ikipata sare mchezo mmoja tu kwa maana ya kupata alama 13 kwenye alama 15 ikiwemo kushinda mchezo dhidi ya Yanga katika ligi.

Msimamo wa Ligi Kuu Bara huku ukionyesha form ya kila timu katika michezo mitatu kabla ya Ligi kusimama kutokan na janga la corona.

Kinachoonekana baada ya michezo minne ya kirafiki kiwango walichokionesha ( standard of play) kilikuwa juu sana. Nimebahatika kuziona mechi tatu kati ya hizo ikiwemo kwenda mazoezini kwao pale uwanja wa Bora Kijitonyama.

Baada ya kocha Hererimana Huruma kuwa muumini wa mfumo wa 4-4-2 huku Kocha msaidizi Habib Kondo akiwa muumini wa 4-3-3 kutokana na aina ya wachezaji walionao KMC “play style” zao zikaswii kwenye mfumo huu moja kwa moja timu ikabadilika kwa asilimia kubwa na ndio hichi tunachokiona sasa.

Hassan Kabunda akimtoa mlinzi wa AS Kigali.

Mfumo huu unafanya timu kuwa na “balance” sana hasa kama una wachezaji wenye kasu kama Kabunda ,Serge na Ilanfya pale juu nyuma yake kwenye “pair” ya watatu wengine ambapo una mtu mwenye uwezo wa kupiga pasi fupi na ndefu kwa wakati moja kama Kenny Ally ,Hassan Kapalata, Abdul Hillary kunafanya ukuta wa akina Ismail Gambo, Kevin Kijiri, Abdallah Mfuko, Ally Ramadhani na mlinda malango mzoefu milingotini Juma Kaseja kutokushambuliwa mara kwa mara kutokana na hii “balance” nzuri iliyopo hasa kwenye utulivu wa kiungo kujenga shambulizi na kutimiza wajibu wa kukaba.

Kevin Kijiri “Kevin Nash” akiwa na Ally Ramadhani “Oviedo”

Mara wanapopoteza umiliki wa mpira si timu nyingi za VPL zinazocheza 4-3-3 kwa maana moja watateseka sana wanapokutana na KMC kama hawatashtukia nini wakifanye dhidi yao toka wameanza kucheza hivyo kila mchezo wanapata goli.

Tusubiri tuone Ligi ikirejea rasmi.

Sambaza....