Blog

Kukaa Benchi la Taifa langu ni ushujaa- Adi Yusuph

Sambaza....

Maneno mengi yanazungumzwa sana kuhusu mshambuliaji wa timu ya Taifa anayecheza soka la kulipwa nchini Uingereza katika klabu ya Blackpool, Adi Yusuph kutopewa nafasi kwenye timu ya taifa.

Lakini yeye mwenyewe anasema kwake yeye kukaa kwenye benchi la timu ya taifa ni ndoto iliyokamilika na ni ushujaa mkubwa sana. “Nimezaliwa hapa nimeondoka nikiwa na umri wa mwaka mmoja. Kwa hiyo nilikuwa na ndoto ya kuitwa timu ya taifa kwa hiyo namshukuru Mungu”.

Add Yusuph akiwa katika uwanja wa nyumbani wa klabu yake mpya

Alipoulizwa kuhusu kuwa mvumilivu wa kukaa benchi pamoja na kutoitwa timu ya taifa amedai kuwa kuna siku atacheza tu. “Inshallah kuna siku nitacheza tu, kwangu Mimi kuitwa timu ya taifa ni good experience na hata wanaocheza wanacheza vizuri na kuna siku nitacheza Inshallah”


-Adi amecheza mechi moja tu akiingia dakika ya 46 kuchukua nafasi ya Farid Musa dhidi ya Algeria katika michuano ya AFCON, mechi ambayo tulifungwa 3-0.-


Adi ataendelea kuja kujiunga na kambi ya Taifa Stars endapo akiitwa. “Nitakuja lazima, kwangu Mimi ni good experience lazima niendelee kuja nikiwa naitwa , nisipoitwa nayo ni vizuri pia”.

Kuhusu yeye kuonekana mhamasishaji mzuri hata kama hapewi namba amedai kuwa hili ni taifa lake. “Hili ni taifa langu, nafurahia kwa sasa tumeenda kwenye hatua ya makundi ya kufuzu kombe la dunia. Kitu ambacho ni kizuri kama taifa , kwa hiyo lazima nihamasishe ili tufanye vyema”

“Uvumilivu tu na kuamini kuna siku utacheza tu inshallah”-alimalizia mshambuliaji huyo wa kimataifa kutoka Tanzania wakati akiwashauri wachezaji kutokususa kucheza timu ya Taifa.

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x