Sambaza....

Coastal Union “Wagosi wa kaya” kutoka Tanga wamerudi katika Ligi Kuu Bara baada ya kushuka daraja misimu miwili iliyopita baada ya kushuka na timu nyingine mbili za Jiji hilo kwa pamoja.

Baada ya kufanikiwa kurudi katika Ligi Kuu Bara wameoyesha ni kiasi gani wamejipanga ili lisiwatokee janga lá kushuka daraja tena.  Wamerudi ligi Kuu wakiwa imara katika uchumi wao wa klabu baada ya kukubali kua mpira pesa.

Coastal Union inapaswa kupongezwa kwa kuweza kuwavutia wadhamini wengi kukubali kutangaza katika jezi zao na kuweza kupata kiasi kikubwa cha fedha.

Hakika mpaka sasa coastal Union ndio klabu inayoongoza kua na wadhamini wengi katika vilabu vyote vinavyoshiriki  Ligi Kuu Bara.

Mofaya, Binslum, TSN ( Tanzânia Sisi ni Nyumbani), GSM, Anjari, Bongo Sportswear ni wadhamini wakuu wa Coastal Union ya jijini Tanga.

Hata ukiitazama jezi ya Coastal Union ama kwa hakika itakuvutia jinsi ilivyo nzuri kutokana na kupambwa na logo nzuri za wadhamini wake.

Hakuna ubishi kwa hili Coastal Union wapo juu kuliko vilabu vyote vya Ligi Kuu Bara. Ndio “Babalaoo katika upande wa udhamini.

Sambaza....