Sambaza....

Wapwa, Ayub Lakred golikipa mpya toka Morocco aliyesajili Simba anakuwa mchezaji wa kwanza raia wa kutoka mataifa ya Kaskazini kucheza nchini Tanzania (kama kuna mtu mwenye data tofauti atatukumbusha)

Kwa kuwa si kawaida kupata mchezaji toka mataifa hayo kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ubora wa ligi zao na uchumi mzuri kwenye ukanda huo kama Tunisia, Libya, Algeria Misri na hawa Morocco kumekuwa na hoja nyingi sana kwake.

 

Mojawapo mashaka kwenye uwezo wake vijiwe vyetu vya ‘gahawa ‘ vina maswali lukuki kwanini atoke kule kuja hapa au la hakuwa anapata nafasi wengine wakadiriki kusema hajacheza muda mrefu.

Ila kiukweli nafasi ya kucheza kwenye kikosi chake alikuwa anapata kubwa tu kwa lugha nyingine waweza kusema alikuwa anaaminiwa. Hata katika mechi zake 10 za mwisho kwenye timu yake kabla ya kujiunga na Lunyasi alipata nafasi yakutosha tena na wapinzani haswa.

Ayoub Lakred

Swala la kwanini yupo hapa au kaacha kule kuja huku kunaweza kuwa na sababu nyingi ndani yake ikiwemo kupata changamoto mpya na kiukweli ndiyo mpira wakulipwa unavyotaka.

Ubishani ukawepo pia baada ya kurejea Manula nini kitafuta ,niseme tunapaswa kusubiri ila nacho kiamini mimi kupitia ushindani ukiwepo kwenye nafasi muhimu kama ile kutafanya kila kipa ndani ya timu kuwa bora hasa hawa wawili watakao kuwa washindani wa moja kwa moja

Sambaza....