Blog

Kwenye Giza la Yanga, Zahera alisimama kama taa!

Sambaza....

 

Muda umepita Baada ya ndoa ya Yanga na Mwinyi Zahera kuvunjika. Ndoa ambayo ilivunjwa wakati ambao hutarajii kuwa itavunjika, huu ndiyo huwa ni wakati mgumu sana kwa pande zote mbili, hasa hasa upande ulioachwa.

Sikuona ajabu kwa Mwinyi Zahera kuzunguka kwenye vya Habari kuelezea taswira nzima ya kilichotokea. Nimekuelewa sana kwa sababu Mwinyi Zahera alisimama Yanga kama kocha kiongozi.

Majukumu yake hayakuishia kwenye Benchi la ufundi peke yake. Hata wakati ambao Yanga ilipokuwa inapitia nyakati ngumu yeye alisimama kama nguzo ili tu Yanga isianguke.

Yeye ndiye aliyetoka mbele ya wanachama wa Yanga na kumwambia ukweli kuwa kwa sasa Yanga ina hali ngumu na ilikuwa inahitaji msaada mkubwa kutoka kwao na kwa sababu Mwinyi Zahera alikuwa anaifanya timu ipate matokeo chanya kuliwapa imani mashabiki.

Mashabiki waliamini kabisa kuwa Mwinyi Zahera alihitaji msaada kutoka kwao, waliamini kama wangemuongezea nguvu basi angefanya vizuri zaidi ya hapo. Walisimama wote kwa pamoja kuzuia Mwinyi Zahera asianguke.

Hata ilipoitishwa Kubwa kuliko , Mwinyi Zahera alikuwa kiungo muhimu sana kuhakikisha inafanikiwa kwa kiasi kikubwa. Kila mtu alikuwa na imani naye , waliamini kumtengenezea timu imara ili tu afanye vizuri.

Wana Yanga walimpenda Mwinyi Zahera , Mwinyi Zahera naye aliwapenda wana Yanga . Akaiona timu kama yake alikuwa tayari kufanya chochote ili kuimarisha timu yake. Hakuwa tayari kushuhudia morali ndani ya timu inakufa.

Hata wakati ambao timu ilipokuwa haijawalipa mishahara wachezaji, mkono wake ulienda moja kwa moja mfukoni ili kuwapoza wachezaji wake. Ndiyo maana walijitoa kwa ajili yake , kila Jasho lilikuwa linatoka kwa ajili ya kumtumikia Mwinyi Zahera.

 

Mwinyi Zahera alihitaji kujenga familia ya ushindi na hali halisi ya timu alikuwa anaijua sana. Hakusita hata kutoa hela ya hotel , chakula au usafiri ili tu timu yake ijione kuwa inamtu ambaye anawajali. Mtu ambaye anawasikiliza kwa kiasi kikubwa.

Leo hii hayupo tena Jangwani , ukame umezidi sana Jangwani . Hakuna maji tena , visima vyote vya maji vimefukiwa na Mwinyi Zahera. Hakuna tena mtu anayejitoa kwa sasa kipindi ambacho mambo yanapokuwa magumu ndani ya Yanga, Giza ni nene na hakuna taa tena ya kulimaliza hilo giza.

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x