Blog

Madame Simba CEO, toka ofisini njoo huku uone.

Sambaza....

MADAM CEO WA SIMBA SPONGA TOKA KWENYE HILO BOX LAKO LA U DIRECTOR PALE UWANJA WA MKAPA UJE UONE UHALISIA WA MAMBO HUKU KWETU KWA ELFU TATU TATU

Dear Madam CEO!

Hope this finds you well!

Anyway achana na hicho kingereza changu cha kutafutia Ugali wa vijana wangu Dwight-Devon na Dwayne-Carter kila siku pahala pangu pa kazi na wala usistuke ukadhani kuna mtu mwingine anataka kutuma CV ya kazi, hilo kwa sasa hapana sioni naweza kuja kutumika pahala gani kwenye timu yangu pendwa, kikubwa tu nimewiwa kukuandikia baada ya kumalizika kwa mechi ya jana kati ya timu pendwa zaidi nchini kwa sasa Simba Sports Club dhidi ya Biashara ya Mara ama kwa hakika ukiachana na kiwango kikubwa kilichooneshwa na Triple C Mwamba wa Lusaka, Luis Miquisone Chinga kutoka Maputo na wachezaji wote wa Simba Sponga kama navyopenda kuliita timu hili lililosheheni kila aina ya vipaji kuna shida kubwa sana ilitokea nje ya uwanja kabla ya kuingia uwanjani kupata burudani ile na hapa ndipo nakwambia toka kwenye hilo Box la ma Directors wenzio uje ujionee hali halisi huku kwingine maana ukiwa uwanjani hasa kwenye Box la Ma Directors pale huwezi jua shida wazipitiazo washabiki wa kawaida.

Jana kabla ya mechi ile kuanza na hata ilipotamatika kumetokea lawama nyingi sana kwenye makundi sogozi lakini pia kuna “voice note” nyingi zinaendelea kutembea kwenye makundi sogozi pia natumaini kwakuwa wewe kwa sasa ni mwanafamilia wa Mpira huu moja kwa moja zitakuwa zimekufikia aidha moja kwa moja kwa simu yako ama kupitia makundi sogozi uliyopo nikiamini hauishi kwenye kisiwa

Mimi nimekuwa na “mixed feelings” kwenye kilichotokea jana upande mmoja nawaelewa walalamikaji lakini upande wa pili napingana nao, na niseme tu hadi nimefikia hatua ya kukuandikia barua hii ya wazi ni kwamba sijachagua upande hadi sasa, hii ni kutokana na kwamba nakiri pande zote mbili zina makosa ila tukirudi kwenye dhana ya MTEJA na TABIA zake basi mtoa huduma anatakiwa kujiongeza sana ili tu sio kutamani kumridhisha kila mteja bali mteja aone kwamba mtoa huduma anajali na kuthamini kile ambacho anakitaka ama anakipata na kukilipia na hapa ndipo ile dhana ya mteja ni mfalme inachukua nafasi kubwa sana.

Katika vitu natamani kukupongeza ni namna mechi ya Simba Sponga vs Biashara United ilivyotangazwa na kushawishi “wateja” Washabiki wengi sana sisemi wale waliokuwa ndani ya uwanja nawazungumzia wale waliokwama nje ya uwanja kupata tickets za kuingia kuitazama mechi ile na kuzua malalamiko mengi sana niseme tu kuna kazi kubwa ilifanywa upande mmoja lakini haikumalizwa upande wa pili na hapa ndipo hasa napotaka kupaongelea kwa mapana yake na nikuombe tu ushike kalamu na karatasi kuya not makundi haya sita ya washabiki wa mpira wa nchi hii na tabia zao makundi haya haijalishi wawe wa Timu yako unayoifanyia kazi ama wa timu pinzani yako kote wapo hivi hivi tu;

Aina ya kwanza ya washabiki ni wale ambao wapo kila siku kwenye Viwanja vya Mpira hapa nawazungumzia washabiki wa aina ya Kaka yangu Mzaramo Ally Mikoi Maarufu kama “Kisugu” hawa ni wale washabiki ambao huwezi kuwakuta hata siku moja wakilalamikia Tickets, huwakuti wakilamaikia utaratibu mbovu wa kuingia uwanjani sababu haya yote wao wanayaepuka mapema sana; hii ni kutokana na sababu kwao kwenda mpirani ni shehemu ya maisha yao ya kila siku, ni experience yaani ni EVENT ni STAREHE kubwa hasa kwao mpira ni kama “ibada ya pili” hawa siku zote watakata ticket zao mapema na mapema tu yaani masaa matatu ama mawili kabla ya mechi utawakuta washaingia uwanjani wanasubiri muda wa mechi ufike na daima aina hii ya mashabiki huwa wanasehemu yao maalum ya kukaa pale uwanjani, hawa siku zote utawakuta uwanjani haijalishi mechi iwe kubwa ama iwe ndogo kundi hili la washabiki wana nafasi ya pekee PEPONI ila sasa shida kubwa ya mashabiki wa aina hii wapo wachache sana hapa Tanzania ukianza kutaja majina utampata Kisugu na Jamaa yangu mwingine wa kuitwa Bebwa tu nikijaribu kuwataja majina

Mashabiki wakifwatilia mchezo wa timu yao katika uwanja wa Taifa.

Aina ya pili ya Mashabiki wetu wa mpira ni wale wanajiita MAKONTAWA yaani WAJANJA wa JIJI hawa siku zote kwao kuingia mpirani ni jambo la dakika 2 tu afike uwanjani dakika 2 aambiwe bei ya tickets 2 alipe na apate tickets dakika 2 kisha aingie uwanjani ndai ya dakika 2 hizo hizo; hawa sasa wapo wengi kuzidi aina ile ya kwanza maana siku hizi hakuna mtoto wa Mama bali kila mtu ni Mtoto wa Mjini kwamba Mjini hakuletwa kazaliwa hapa hapa japo wengi tunawajua kwao ni Msanga na wengine kutoka Muleba Kaskazini huko ila fresh tu tunaishi nao, aina hii ya pili ni ngumu kuibadilisha hii ni hulka ngumu sana ku-deal nayo japo sisemi hauwezi kuwabadili as a matter of fact kuna muda na rasilimali za kufanya hivyo zikiwepo basi unaweza kuwapata asilimia fulani.

Aina ya tatu ya Mashabiki hii sasa ni wale ambao mpira kwao sio kitu cha kuwekwa kwenye ratiba yao hawa siku zote huwa wanafanya kitu sababu kamuona Fulani anafanya, kamuona Kisugu ama kamsikia kisugu anaelekea uwanjani basi na yeye ataamua muda huo huo kuelekea uwanjani hawa ni aina ya watu ambao maamuzi yao siku zote huwa yanaathiriwa na kitu tunaita “Mob Psychology” hawa sasa ukichanganya na hao MAKONTAWA tunaanza kuzalisha tatizo kidogo kidogo la watu kujaa pale uwanjani na kuanza kutafuta wanapokatia tickets.

Aina ya nne ya Mashabiki ni wale ambao wao siku zote huwa wanalalamikia mfumo, hawa sasa huwa wanatafuta kila eneo lenye madhaifu wakuhukumu nalo wao siku zote husubiri muda wa matatizo ndio waibuke, hawa hawapo tayari kukata tickets zao mapema sababu huwa wanasubiri mambo yachache wapate cha kuongea, wapate sehemu ya kumalizia stress zao hawa siku zote wanasema wapo busy na mambo yao na kauli mbiu yao kuu Tickets sio jambo la kumfanya achelewe ama akose kutazama mpira pale anapoamua kufanya hivyo, nafikiri hadi hapa ushaelewa ni makundi mangapi yanakuja kuzalisha lile tatizo la jana lililotokea na kuzua taharuki kubwa pale nje ya Uwanja wa Mkapa tatizo ambalo limeleta shuida kubwa.

Aina ya tano ya Mashabiki hawa siwezi kuwaita Mashabiki bali jina lao sahihi niwaite “WATU WAPYA KWENYE MPIRA WETU” hawa ni wageni wakija uwanjani hawa wakimwagiwa maji wanataka kupigana, Uwanja ukiwa umejaa ukimwambia sogea kidogo tujibane anakwambia ungewahi sasa kwenye biashara hawa naweza kuwaita wateja wapya, wanaweza kuwa na Ushabiki na timu lakini huwaoni uwanjani, hawataki kuja sio kwasababu hawazipendi timu hapana hawaji sababu hawaoni sababu ya kuwafanya kuja viwanjani siku zote hawa wanakuja kufata “Event” mfano Simba Day ama mechi ya Simba na Yanga, yawezekana kuna swali huwa unajiuliza wako wapi wale watu wanaoujaza Uwanja kwenye Simba Day? Ama wale wanaoujaza Uwanja kwenye Derby ya Kariakoo? Jibu ni moja tu hawa wanakuja kufata EVENT kubwa iliyotengenezwa kwa namna ambayo imewashawishi kwenda uwanjani ili tu abaki na simulizi za kusimulia mfano nilikuwepo uwanjani siku Mtani anapigika MKONO, kwa kawaida hawa huwa ni wengi kuliko wote niliowataja hapo kabla

Aina ya sita na ya mwisho hawa tunawaita wazee wa GANDA LA NDIZI siku zote wao huingia uwanjani BURE na huwa wanausemi wao Mpira unachezwa vipi sasa kama mimi sipo ndani ya Uwanja? Hawa kwa sasa nakuomba TUWAPUUZE maana sio wengi sana kuyazidi hayo makundi mengini niliyotangulia kuyataja.

Naweza kukubali kweli ni ngumu sana ku strike the balance kati ya huduma bora na gharama za chini zilizotozwa siku ya jana lakini pia huwezi kukubali ku make tradeoff kwamba utaamua kwenda na washabiki wachache wenye wenye kujitoa mapema kabla ya chochote na kuachana na pesa tulizopoteza jana kama mapato sababu tu washabiki wale ambao nataka tuwaite Prospective Loyal customer sababu tu walikuja kwa kuchelewa mapato ambayo kama Klabu pengine tungeweka rekodi kwenye ligi kuu kwa mechi isiyohusisha Simba SC vs Yanga SC ama Simba vs Azam FC kuingiza watu wengi zaidi kwa washabiki ama wateja waliokuja kuitaka huduma yetu dakika mbili kabla hatujafunga ofisi kwa kwisha kwa muda wa kazi, niseme tu inawezekana ukawa unajua zaidi yangu sawa ila kwa sasa naomba upoteze muda wako kusoma hiki nilichokuandikia nia ikiwa ni kujenga na kukukumbusha kwamba kuelekea kwenye Mechi vs Biashara niliona namna ya Matangazo yaliyofanywa kuanzia wachezaji hadi mashabiki, vikundi vya ushangiliaji hadi mabosi wa Simba Sponga, kuazia Makundi Sogozi hadi Social media za Klabu mwisho tumalizie na Tv na Radio kwa namna mlivyotangaza niliona mnaenda kutengeneza Event nyingine kubwa sana pembeni ya Simba Day ama pembeni ya Simba na Yanga ila niwachane tu mlichukulia poa kwenye maeneo mengine hasa hasa yale ya kutoa huduma ya moja kwa moja kwa mteja ambae ni mshabiki.

Nasema mlichukulia poa sana sababu sikuona Jitihada zenu hasa baada ya yale yaliyotokea baada ya Simba Day ambapo tickets zilianza kuuzwa siku moja kabla ya Event ile kiasi kwamba kuliibuka shida kubwa sana kwa washabiki ambao ndio wateja wa moja kwa moja wa bidhaa ya klabu ambayo ni mpira kuteseka sana kupata zile tickets, lakini pia mfumo uliokuwa unatumika ulikuja kama upepo kwa maana ya kutumika kwa mara ya kwanza kwenye Tukio kubwa la Ki-Nchi hakukua na fall back plan yoyote ili kuokoa kadhia yoyote ambayo pengine ingeibuka zaidi ya kutaka kumuondoa vendor mpya na kumleta Vendor wa zamani a-chip in na yeye aanze kuuza tickets kitu ambacho mligomewa yote haya sio ishu kubwa kwangu; ISHU Kubwa sana kwangu ni namna mlikosa hata chembe ya Aibu kuja kutuomba radhi sisi wateja wenu kwa kadhia ile, na hapo ndipo nasema MLITUCHUKULIA poa!

Kwa tukio la jana SITAKI kukufanya uje kutuomba Radhi la hasha lakini natamani kukusikia ukilisemea aidha kwa vyombo rasmi vya habari ama kwa social media zetu kwa namna gani mnaweza kulitafutia ufumbuzi wa muda mfupi kwa kulipunguza ama kuliondosha kabisa siku za usoni ila kukaa kwenu kimya hadi sasa kunamaanisha ile nguvu yenu kubwa ya matangazo ilikuwa ni bure kabisa; ni bure sababu Klabu imeendelea kukosa mapato sababu washabiki walifika uwanjani lakini walishindwa kuingia uwanjani sababu hawakuwa na tickets mikononi mwao na nyinyi mmekaa kimya mkisubii mje tena mara nyingine mtupigie kelele zile zile then kwa tabia ile ile toka kwa wateja wale wale tuendelee vile vile kusikia kelele zile zile.

Kitu kingine cha kusikitisha natamani kukusikia ukizungumza ni vipi mtoa huduma awe analalamikiwa sana tena kwa mara ya pili mtawalio hasa kwenye event ndogo kama ya jana huku nyinyi mkiendelea kukaa kimya, katika hali ya kawaida kabisa niseme watanzania sisi tunajuana linapokuja suala kupangilia mambo yetu lakini kwa kilichotokea jana pale Taifa Klabu inapokea lawama zake lakini pia Mtoa huduma anapokea lawama zake, na hata mshabiki pia anapokea lawama zake ila kwa kuwa mshabiki ni mteja ambae tunaitaka sana presence yake tukubaliane kumvumilia kwa madhaifu yake huku tukipambana kumtengenezea mazingira rafiki sana siku za usoni huko ili abadilishe mtazamo wake juu ya namna bora ya kupata huduma yetu, so ningependa tuanze na Klabu wakati mnatangaza kiingilio kuwa elfu tatu hukumwambia mteja wako kwamba katika bei hiyo haitajumuisha bei ya kadi hivyo kumfanya mshabiki wako kwenda na elfu tatu yake pale uwanjani kama ujuavyo maisha ya watu wa daraja la chini halafu anafika pale uwanjani anaambiwa anapaswa akanunue kadi kwanza kwa elfu moja kwenye point tofauti na kisha aje kwenye point ta ticktes ili awaze kununua ticket; hapa kwenye elfu tatu kuwa elfu nne kwenye eneo la tukio mlifanya Uhunimkubwa sana usioweza kuvumilika whether mlikua mnajua or mlikua hamjui!

Lawama za upande wa mtoa huduma hasa wale wakatisha tickets nafikiri ni wale wale watoto wa mjomba na shangazi hawajui nini wanapaswa kufanya kunapotokea taharuki kubwa kama ya jana, hawana customer care, hawama lugha nzuri ya biashara, yaani ile jana Mteja kapandisha mori kama Mmasai mtoa huduma anajifanya ana hasira kama Mkurya mwisho wake wakaanza kutukanana na washabiki ambao wao wanaamini ni haki yao kuipata huduma bora ya mtoa huduma ambae ameshindwa kazi yake na kuibua kadhia kubwa huku mtoa huduma akiamini kama mteja yule angekuwa na haraka angewahi toka jana yake ilia pate ticket; kwenye hili mimi kama mimi naamini hata wewe kwenye maisha yako ya kawaida ukimuona mtoa huduma wako hafanyi vyema utamuhama mara moja ila sasa kwa washabiki wa mpira hali ni tofauti wanakuja kuifata Starehe ambayo wanailalamikia katika kuipata na mwisho hawaipati kabisa ama wanaipata kwa kuchaniana mashati na jezi walizovaa sababu hakuna mtoa huduma mbadala wa kuikidhi haja ya mioyo yao!

Mtoa huduma analalamikiwa pia kwenye baadhi ya vituo mfano Tegeta hakukuwa na huduma kwa wakati, lakini pia mtoa huduma hana rasilimali watu, ama rasilimali vifaa vya kutosha kukabiliana na Unforeseen event ama boom, hapa niseme tu kwa namna mlivyotangaza, na kwa namna mlivyoshusha bei nafikiri mlipaswa kuliona hili mapema kabisa huku mkijumlisha na tabia za washabiki wetu huwa wanakata tickets zikiwa siku ya tukio na zikiwa zimebaki dakika 10 ama masaa mawili kabla ya mpira kuanza kifupi hawana mazoea ya kufanya maamuzi mapema na katika kubariki ujinga huo wa kimazoea bado mtoa huduma na timu yangu mlikubali kuendelea na Utumwa ule na kuleta tickets viwanjani na kuuza ili tu msizikose zile pesa matokeo yake mkaishia kujitukanisha tu kwa kushindwa kutoa huduma dhahaniwa na wateja, niseme tu hili halina afya kwa mustakabali wa mpira wetu lakini pia kwa mustakabali wa klabu yetu hasa klabu mwenyeji wa mechi ikumbukwe klabu mwenyeji ndio anabeba mapato yote!
SWALI hivi mshajiuliza kwanini Vilabu vya mikoani kila mwaka wanapiga kura mwenyeji wa mechi aendelee kuchukua mapato yote? Jibu rahisi sana sababu ni moja tu wanajua wakija hapa Dar es salaam mwenyeji hanufaiki kwa mapato kama vile wanayoyapata wao huko mikoani pindi Timu zetu zinapoenda huko kutokana na namba ya watazamaji huwa chache kulinganisha na namba ile wanayopata kule mikoani, ukijumlisha na makato ya mechi husika, lakini kama ingekuwa tunapata walau mechi 15 tu za msimu wa Ligi kuu na kupiga full house pale kwa Benja hivyo vilabu vya mikoani vingejitafakari lakini wao wanaamini Simba ikienda Morogoro pale Mtibwa ataachana na Uwanja wake aidha wa Manungu ama Gairo na kuja kuutumia Uwanja mkubwa wa Jamhuri sababu wana uhakika watu watajaa pale Jamhuri na wengine watabaki nje ya uwanja kwa kuuziwa tickets lakini watakosa kuingia sababu uwanja utakuwa umejaa ila wao watakuwa washaingiza pesa ile hili lilitokea pale Arusha mechi ya Ufunguzi wa Ligi kati ya Simba vs Namungo!

Madam CEO natamani ulijue hili Simba inayoenda Mkoani mara moja tu kwa mwaka tena hasa Simba hii ya sasa ilivyo ya Moto nafikiri unadhani Waluguru wenzangu wata Plan kuikosa EVENT hiyo? Abadani asilani hawatokosa sababu watajua wakiikosa basi itawalazimu kusafiri mikoa ya jirani; Basi hii ndio sababu kwanini Mikoani Viwanja vinajaa wakati hapa Dar hatufikishi hata robo ya uwezo wa uwanja mkubwa ambao tungeutumia kama rasilimali yetu kubwa tungevuna kipato kikubwa sana, watu wa Dar wanajua kwa msimu ana Mechi (EVENT) Tano za kutazama nazo ni Simba Day then Simba vs Azam mbili na Simba vs Yanga mbili hizi kwao ni EVENT ambazo hata kama hatupigi makelele sana tutapata washabiki wa kuja kututazama!

Nilikuwepo nchini Lesotho siku Tanzania tunacheza vs Lesotho pale Maseru mechi ya kufuzu kwa AFCON iliyofanyika Misri; ilikuwa mechi ya kushangaza kwa upande wa Mashabiki hadi tunaingia uwanjani saa tisa na robo alasiri kwa saa za pale Lesotho ilikuwa uwanja mtupu lakini hakuna sehemu yoyote niliona pale nje ya uwanja wakiuza Tickets lakini wakati ulipofika dakika 10 kabla ya mechi kuanza Uwanja ulikuwa ushajaa kitu nilichojifunza pale Tickets zinauzwa na Vendor Mmoja wa kuitwa Shoprite so ili upate Match Day Ticket ilikupasa uende Shoprite, pale shoprite kulikuwa na usalama mkubwa sana wa mtoa huduma kwa maana ya pesa zake lakini pia kwa mpata huduma ilikuwa rahisi sana kupata huduma na watu wa Taifa lile wameupokea utaratibu ule na wanauishi fresh tu, walipokuja uwanjani tulishindwa kutofautisha maana walikuja Baba, Mama na watoto wao wa Kike na kiume, walikuja Mabinti wa umri wa kati na Wavulana walikuja Machizi mpira na hata wengine wengi ambao ungeweza kushangaa kuwaona kuja viwanjani kwetu sababu kubwa ni kwamba kwao Mechi za mpira wa miguu wamezifanya kuwa MATUKIO YA KIFAMILIA kupata mtoko wa siku!

Ukiwa unakuja Tanzania na ukakuta Simba Day ama Siku ya Mwananchi ama hata Dar Derby na ukiwa mgeni utasema vilabu vya nchi hii ni matajiri sana sababu wanaishi na watu wanaoupenda mpira sababu utasikia mechi imeingiza milioni mia tano sasa ukiwaza kwenye nadharia timu hizi zikicheza mara 10 inakuaje? Na hapa sasa katika kuu-deceive ulimwngu kitu pekee ambacho huwa tunafanya ni kushea picha za matukio hayo mitandaoni kiasi kwamba majirani zetu huwa wanatamani waje hapa na kuwa sisi, lakini ukweli ni kwamba ukiondoa mechi hizo mbili ama matukio hayo ukweli ni kwamba huwa hatupati watu wengi viwanjani kwenye mechi nyingine zaidi ya hizo mbili ama matukio hayo mawili tu na Dar es Salaam ndipo kunakuwa na namba ndogo zaidi ya washabiki viwanjani pengine kuliko za Mikoani kwa mechi zinazohusisha Simba na Yanga vs timu hizo za mikoani pengine ni sababu ya mambo mengi ambayo wahusika hamfanyi nje ya uwanja na kubaki mkiishi kwa mazoea ya wateja wale wale akina Kisugu Mikoi mmegoma kutoka nje ya boksi la u Director mlilojifungia, huku mkiwa hamtaki kupigania kuwabadilisha mitazamo wale “wateja” wenu wa namba mbili, tatu, nne, tano na sita niliowaaninisha!

Kwangu naamini ni mchakato lakini bora kuunza sasa kuliko kuendelea kuamini tuko vizuri kwenye makaratasi kuliko kuwa halisia on the ground; kadhia iliyopatikana jana iwe fundisho kwenu na katika nadharia ile ile kwamba licha ya Apple kuwa ndio kampuni inayoongoza kwa sasa kwenye vifaa vya ki-Electronics lakini kila siku wanapambana kupata wateja wapya, kila siku wanapambana ku retain existing customers wao kila siku wanafanya wateja wao waone bidhaa zao sio tu bidhaa bali ni maisha yao ya kila siku wanayopaswa kuyaishi, ndivyo vivyo hivyo mteja huyu wa klabu yetu, pamoja na Mapenzi yake kwa timu, pamoja na kuvutiwa na mpira mzuri wa Chama Jr uwanjani basi na pale anapotaka kuyaishi haya mazuri na mapenzi yake tumtengenezee mazingira rafiki kwake, mazingira ambayo sio tu kwamba atakutana na Bank Hall nzuri, kuna Kiyoyozi cha kutosha, kuna space kubwa na verandah nzuri ya kuvutia lakini huduma mbovu mteja huyu hawezi kusumbuka kuja tena na tena kwako!

Jana kuna watu zaidi ya elfu 10 walikuja uwanjani kwa mara ya kwanza pengine sababu walimuona Chama akizungumza kwenye zile video zilizagaa kwenye makundi sogozi akiwaambia njooni nyote uwanjani kuna kitu kikubwa kinaenda kutokea, labda mshabiki yule alikuja sababu aliambiwa tickets ni elfu tatu akawaza yaani kumuona live Miquisone ni elfu tatu tu kwanini nisiende? Labda mshabiki yule alikuja uwanjani baada ya kupambana sana kuvunja ahadi ambazo zilimtaka kuzitimiza, labda alikuja uwanjani sababu aliona wenzie wote wakizungumzia mpira akasema acha niende huko lakini kwa alichokutana nacho jana kupoteza muda, pesa na mwisho kabisa kushindwa kupata kuona kitu kilichosababisha avunje kila ahadi yake ukimuuliza leo hii kama bado ana tamaa ile ile atakwambia maishani sitakaa kwenda mpirani tena! Hapa tumeshindwa kumtengeneza loyal customer mwingine pembeni ya Kisugu hii ina maana Mshabiki yule ataendelea kubaki kutazama mechi kwenye TV kitu ambacho ni rahisi kwake kufanya ikipelekea Timu ikiikosa pesa yake ile ya moja kwa moja!

Naomba nisikuchoshe Madam CEO maana nina mengi sana lakini ukipata wasaa nikuombe utoke nje ya hilo Box lenu la Ma Directors pale uwanjani, hebu toka hata mara moja njoo uwaone wateja halisi wa Timu yako wanavyopata taabu kupata kuiona raha ya kumuona Chama live uwanjani, toka kwenye hilo Box la ma directors wenzio uje ku experience hicho kiingilio cha chini mnachosema mmepa mtu wa hali ya chini namna kinavyomtesa hadi hatamani kiendelee kuwapo, Madam CEO ikuombe tena utoke kwenye lile box la ma directors wenzio uje kutuomba msamaha kwa kilichotokea Simba Day, na pia uje utuombe msamaha kwa kile kilichotokea Jana na kutuahidi hakitatokea tena huu ni Msalaba wako Madam CEO huukwepi

Madam CEO toka hapo uliposimama kwa kuamini kila kitu kitafanyika kwa kutumia Remote; kumbuka kwamba CUSTOMER IS ALWAYS RIGHT njoo tuzungumze ukiwa umeondoa kwenye kichwa chako MSHABIKI ANAPASWA KUIPENDA TIMU YAKE NA KUICHANGIA KWA KIINGILIO CHAKE UWANJANI; Madam CEOtoka kwenye hilo SHIMO ASAP huna namna nyingine

Madam CEO toka sasa kwenye Box lako la U Director maana wakati ni huu na SISI WASWAHILI TUNASEMA USIPOUANIKA UTAULA MBICHI

Haya ndio pekee naweza kuyasema kwa sasa kwako Madam CEO

Best regards;

©️Mdidi kama Mdidi the Writer😎

Sambaza....