Blog

Madhaifu mawili ya Simba yaliyoanikwa na Sevilla

Sambaza....

Juzi kulikuwa na mechi ya kihistoria kati ya Simba ya Tanzania na Sevilla ya Hispania katika uwanja wa taifa. Mechi ambayo itabaki katika kumbukumbu ya watu wengi. Lakini mechi hii ilionesha madhaifu yafuatayo kwa Simba .

HAINA KIKOSI KIPANA KIMATAIFA

Moja ya vitu ambavyo Simba ilikuwa inajivunia kwenye ligi kuu ni kuwa na kikosi kipana ambacho kiliwawezesha kushinda mechi ambazo zilikuwa viporo.

Walikuwa wanacheza kila baada ya siku mbili, lakini walifanikiwa kupigana mpaka wakapata alama ambazo ziliwasaidia kutetea kombe lao.

Kitu hiki ni kizuri kwa Simba, lakini Simba wanaenda kwenye michuano ya kimataifa, wanatakiwa kujenga kikosi ambacho kina sura ya upana wa kimataifa.

Baada ya kipindi cha kwanza Simba kuanza na kikosi chao halisi , na kipindi cha pili kuingiza kikosi cha pili na kikashindwa kuhimili mechi ukilinganisha na kikosi cha kwanza. Hii ilionesha Simba wana kikosi kikubwa kwenye ligi kuu na siyo kwenye mechi za kimataifa.

UDHAIFU KATIKA MIPIRA ILIYO KUFA

Moja ya makosa ambayo Simba imekuwa ikiyafanya hasa hasa kwenye mechi za kimataifa , kuanzia kwenye michuano ya klabu bingwa Afrika na kwenye mechi ya Sevilla yalijirudia ni udhaifu wa kuzuia mipira iliyokufa.

Mabeki wa Simba hawajui kujipanga vizuri kwenye kuzuia mipira iliyokufa (kama kona na faulo) na wamekuwa wakifanya makosa mengi kwenye mipira iliyokufa.

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x