Sambaza....

Leo Taifa Stars inacheza mechi ambayo itaamua uwezekano wa wao kushiriki Afcon ya mwaka 2019 huko Cameron. Wanahitaji ushindi ambao utawahakikishia safari ya kwenda Cameron.

Kama wakishinda watakuwa wamefikisha alama 8 ambazo haziwezi kufikiwa na Cape Verde pamoja na Lesotho. Hivo watakuwa wameungana na Uganda moja kwa moja kwenda Cameron.

Maeneo yapi ambayo yanaweza kuifanya Taifa Stars ishindwe kushinda mechi ya Leo ?

UWANJA WA UGENINI.

Katika kampeni hizi za kufuzu kwenda Afcon, Taifa Stars mpaka sasa haijashinda mechi ya ugenini kwenye mechi mbili ambazo wamecheza ugenini. Walitoka suluhu Katika uwanja wa Nambole nchini Uganda, na wakafungwa goli 3-0 nchini Cape Verde. Takwimu za mechi za ugenini haziibebi sana Taifa Stars.

Msimamo wa kundi (Livescore)

LESOTHO WANA NAFASI YA KUFUZU.

Mpaka sasa Lesotho wana alama mbili, na wamebakiza mechi 2 kama wakishinda mechi zote mbili watafikisha alama 8, alama ambazo zinawapa nafasi kubwa wao kufuzu kwenda Cameron. Hivo ugumu wa mechi ya leo kwa Taifa Stars unaanzia hapa kwa Lesotho kuingia uwanjani kama watu ambao wanahitaji nafasi ya kufuzu na siyo watu ambao wamekuja kukamilisha ratiba.

UKOSEFU WA MBWANA ALLY SAMATTA.

Katika kampeni hizi za kufuzu kwenda Afcon, timu ya Taifa Stars imefunga magoli 3, magoli ambayo yote kwa 100% Mbwana Ally Samatta kahusika kwenye magoli hayo. Hivo leo hayupo akitukimikia adhabu ya kadi mbili za njano. Taifa Stars wanaingia bila ya mtu muhimu Katika upatikanaji wa mabao. Hii nayo inaweza ikasababisha Taifa Stars wasishinde mechi ya leo

Sambaza....