Blog

Majaribio ya Wachezaji Jinsia Zote Umri Miaka 6 – 20

Sambaza....

Ivo Mapunda sports center kwa kushirikiana na chama cha soka mkoa wa dar es salaam (drfa) kwa pamoja wanakuletea majaribio ya wachezaji jinsia zote mwezi wa kwanza mwanzoni wa mwaka 2018 kwa wachezaji kuanzia umri wa miaka 6 – 20.

Mchezaji ili aweze kushiriki majaribio haya anatakiwa kujaza fomu ambayo ataipata katika vituo tajwa hapo chini kwa bei ya tsh 5000 ambayo ipo ndani ya kitabu cha soka ambacho kinaitwa “boresha na endeleza kipaji chako cha soka” kinafundisha mchezo wa soka pia kitamsaidia mchezaji kujiandaa na majaribio na kuwa mchezaji hodari hapo baadae.

Fomu itapatikana sehemu zifuatazo
1. Ofisi zote za vyama vya wilaya vya soka, ilala, ubungo, kinondoni, temeke na kigamboni.
2. Kimara mwisho – kituo cha mabasi sehemu ya gazeti kuelekea mjini.
3. Tabata shule – kituo cha basi sehemu ya gazeti kuelekea mjini.
4. Banana – kituo cha basi sehemu ya gazeti kuelekea gongo la mboto.
5. Magomeni kanisani – kituo cha basi sehemu ya gazeti kuelekea mwananyamara.
6. Mwenge – kituo cha basi sehemu ya gazeti kuelekea tegeta.
7. Mbagala zakhem hospitali – kituo cha basi sehemu ya gazeti kuelekea rangi tatu.
8. Pamoja na mawakala watakao pita mitaani.

Mahali pa kufanyia majaribio utafahamu kwa kuangalia kwenye fomu kwa kila wilaya, viwanja, siku na muda.
Fomu zitaanza kupatikana tarehe 8 / 12 /2017 mpaka tarehe 05/ 01/2018. Siku ya majaribio mchezaji unatakiwa kuja na fomu pamoja na kitabu ili uweze kufanyiwa majaribio.
Siku ya majaribio kutakuwa na vituo na timu zifuatazo zitakazo angalia uwezo wako na kukuchukua
1. Ivo mapunda sports center – kituo hiki kina shirikiana na baadhi ya timu za afrika mashariki.
2. Shadaka 20 – kampuni hii inajihususisha na kuwatafutia wachezaji timu na vituo vya kuendeleza vipaji vyao sehemu mbalimbali duniani, inamilikiwa na shaffih dauda.
3. Kinondoni rangers sports academy – kituo ambacho kinasifika kwa kukuza vipaji vya soka nchini.
4. Lord baden high school – shule ya kanali mstaafu idd omary kipingu atakupunguzia ada na ikibidi utasoma bure katika shule yake ya michezo.
5. Pia zitaalikwa timu zinazoshiliki ligi kuu tanzania bara na visiwani kama simba, yanga na azam.


Pia kutakuwa na zawadi za vifaa vya michezo kwa wachezaji watakao fanya vizuri kwenye majaribio.
Haya majaribio hayajawahi tokea tanzania: mzazi mlete mwanao, mchezaji njoo uonekane na mwalimu ilete timu yako kwani mchezaji akichukuliwa haki yako utapata. Kwa maelekezo zaidi 0717 100042


Sambaza....