La Liga

Mambo matano yanayoitafuna RealMadrid

Sambaza kwa marafiki....

Waliokuwa mabingwa watetezi wa ligi ya mabingwa barani ulaya, Rwal Madrid,  ubingwa ambao waliuchukua mara ya tatu mfululizo na ndiyo ubingwa ambao Ajax wamemtemesha. Real Madrid kwa msimu huu wamekuwa na msimu usiyo bora kwao wao na wamekuwa wakifanya vibaya ukilinganisha na misimu mingine mitatu nyuma.

Mpaka sasa hivi hawana uhakika wa kuchukua kombe jingine baada ya wao kuchukua kombe la ligi ya mabingwa dunia. Copa Del Deley wameshatolewa, La Liga wana nafasi finyu na ligi ya mabingwa barani ulaya wameshatoka. Lipi tatizo linalowakumba?

KUTOKA KWA ZIDANE , KUINGIA KWA JULAN LOPATENGUE NA SOLARI

Zinedine Zidane alikuwa ameibeba timu, alikuwa amebeba molari ya timu kushindana. Alipotoka akaingia Julan Lopatengue molari ikawa siyo kubwa kama kipindi kile ambacho Zidane yupo, Solari naye kapata nafasi lakini mpaka sasa hajafanikiwa kuingiza molari ya ubingwa ndani ya wachezaji.

KUTOKA KWA RONALDO

Hapana shaka hili ni pengo kubwa ambalo ni ngumu kulikataa, binadamu ambaye alikuwa na uwezo wa kufunga magoli kuanzia 30 na kuendelea ndani ya msimu mmoja. Mpaka sasa mchezaji anayeongoza kwa magoli ni Karim Benzema mwenye magoli 11, Bale 7, Ramos 6, Casemiro 3. Wakati Ronaldo alikuwa na uwezo wa kufunga magoli kuanzia 20 nyakati kama hizi huku mtu ambaye aliyekuwa anamfuata ndani ya klabu akiwa na magoli hata 15.

KUSHUKA KWA KIWANGO KWA TONI KROOS na LUKA MODRIC

Hawa kwa kipindi kirefu wamekuwa mhilimili mkubwa kwa timu ya RealMadrid, lakini kwa msimu huu wamekuwa na kiwango ambacho siyo kikubwa sana ukilinganisha na misimu kadhaa nyuma. Mpaka sasa idadi ya magoli kwa pamoja waliyofunga hawa haizidi magoli mawili.

USHIRIKIANO WA UFUNGAJI MAGOLI

Kwa kipindi cha nyuma enzi za Zidane kuna baadhi ya wachezaji walikuwa wanahusika sana katika ufungaji wa magoli hata kama Ronaldo asipofunga. Mfano, Casemiro, Ramos, Marcelo walikuwa wanahusika na ufungaji wa magoli lakini kwa msimu huu wamekuwa hafifu sana kwenye hili suala.

KUSHUKA KIWANGO KWA MARCELO na DANI CARVAJAL

Hawa walikuwa funguo ya mashambulizi ya RealMadrid, ambapo magoli mengi yalikuwa yanatokea pembeni ambako walikuwa wanacheza lakini kwa msimu huu imekuwa tofauti. Hawazalishi tena magoli kwa kiwango kile cha mwanzoni.

Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.