Kombe la Dunia

Mechi Iliyoamua mshindi hatua ya Makundi Kombe la Dunia

Sambaza....

Hii ilikuwa ni Kombe la Dunia mwaka 1950, mechi ya Uruguay dhidi ya Brazil. Mechi ambayo iliamua mshindi hatua ya makundi. Uchambuzi huu umeaandaliwa na Maka Patrick Mwasomola, Chef kutoka FQ Hotel ya jiji Dar ea Salaam.

Wasomaji wapendwa, mabibi na mabwana habari za wakati huu.

Bado tunaendelea na habari za bara la Amerika ya Kusini.

Baada ya kuona harakati za wanamapinduzi wawili wasaidizi wa Ernesto Che Guevara, mwanamama Haydee Tamara Bunke maarufu kama “Tania The Guerrilla” mwanamama huyu Mjerumani mzaliwa wa Argentina ambaye pia alikuwa raia wa nchi hiyo pamoja na Simeone Cuba Sarabia maarufu kama Willy, raia wa Bolivia na namna harakati zao zilivyofikia tamati mwaka ule wa 1967 kule nchini Bolivia, leo tunarudi tena Amerika ya Kusini lakini nyuma miaka kumi na saba kabla ya tukio lile la kina Che Guevara nchini Bolivia mwaka 1967.

Tunaenda kuzungumzia tukio la mwaka 1950. Lakini hatuendi kuzungumzia harakati za Che Guevara na washirika wake bali tunaenda mpaka nchini Brazil na kuzungumzia fainali ya kukata na shoka ya Kombe la Dunia la FIFA kati ya Brazil na Uruguay iliyofanyika mwaka huo katika uwanja wa Maracana.

TeamPldWDLGFGAPts
 Brazil22001324
 Uruguay2110543
 Spain2011381
 Sweden20023100

Hapo siku za nyuma kidogo niliwahi kuandika kuhusu Alicides Ghiggia, “Jini” winga wa Uruguay aliyepeleka kilio katika Brazil nzima siku hiyo ya fainali.

Leo tunaenda kulizungumzia kwa kirefu pambano lenyewe na namna lilivyokuwa na matumaini kwa Celecao kuwa mabingwa wapya wa Kombe la Dunia, makosa ya kujiamini kupita kiasi kama hayo walikuja kuyarudia tena mwaka 2014, wakati Kombe la Dunia la FIFA liliporudi tena katika nchi ile kubwa kule Amerika Kusini, nchi iliyotawaliwa na wakoloni wa Kireno zamani, Brazil.

Kama nilivyokwishakutangulia kusema hapo juu kuwa mechi kati ya Uruguay na Brazil ilikuwa ni mechi ya kuamua fainali katika hatua ya makundi katika Kombe la Dunia la FIFA mwaka 1950. Mechi hiyo ilichezwa katika uwanja wa Estádio do Maracanã katika mji mkuu wa Brazil wa wakati huo wa Rio de Janeiro tarehe 16 Julai, mwaka 1950.

Tofauti na fainali nyingine za Kombe la Dunia, bingwa wa mwaka 1950 alipatikana kutoka katika hatua ya makundi, kwa timu nne za mwisho kucheza kwa muundo wa pande zote, badala ya hatua za mtoano. Huku Brazil ikiwa pointi moja mbele ya Uruguay kuelekea mechi hiyo, Uruguay ilihitaji kushinda wakati Brazil walichohitaji tu wao ni kuepuka kipigo ili watangazwe kuwa mabingwa wa Dunia.

Brazil ilipata uongozi wa mchezo muda mfupi tu baada ya mapumziko kwa goli lililofungwa na Friaça, lakini Juan Alberto Schiaffino aliisawazishia Uruguay katikati ya kipindi cha pili. Alcides Ghiggia alifunga bao la ushindi zikiwa zimebakia dakika 11 mechi kumalizika, iliyopelekea kuwa mojawapo ya matokeo ya kusikitisha sana katika historia ya mchezo wa mpira wa miguu, na kupelekea jina Maracanazo au Maracanaço, linalotafsriwa kama “Balaa la Maracanã” likichukua jina la uwanja wa Maracana na kuwa kifupisho cha mechi hiyo. Mechi hiyo ilikuwa ni ya pili (na mpaka sasa, ya mwisho) kwa mechi ya finali kuzikutanisha timu mbili kutoka Amerika ya Kusini (ya kwanza ikiwa ya mwaka 1930 fainali kati ya Uruguay na Argentina, ambayo nayo Uruguay ilichukua ubingwa).

Ghiggia alikuwa mchezaji wa mwisho wa mechi hiyo ambaye alikuwa amebakia hai; alifariki tarehe 16 Julai mwaka 2015 (miaka 65 kamili baada ya kufunga goli muhimu), alifariki akiwa na umri wa miaka 88.

ITAENDELEA………

Sambaza....