Sambaza....

Manchester City ilianza harakati zake za ubingwa msimu huu kwa kudroo na Everton tena nyumbani Etihad kabla ya kurudi na kukaa sawa na kuifunga Bournemouth ugenini.

Ligi ya Uingereza inayosifika kwa soka la kibabe na nguvu lilishindwa kufua dafu mbele ya Guardiola aliekuja na “soft football” na kutangaza ubingwa mapema tuu.

Pamoja na kuchukua ubingwa wa EPL lakini kuna mechi ambazo hakika zilikua ngumu kwa Manchester City na kuwafanya kukomaa walau kupata point tatu au moja kabisa.

Mechi za ubingwa za Manchester City: 

Man U 1 vs Man city  2

Mchezo ulipigwa katika uwanja wa OT magoli ya David Silva na baadae Nicholas Otamendi kufuta lile lá kusawazisha lá Marcus Rashford liliipa Man city point tatu muhimu. Sii tuu City walipata point tatu lakini pia walimfunga mpinzani wao na mshindani wake wa ubingwa.

Image result for manchester city vs manchester united 2018

Newcastle 0 vs City 1

Katika uwanja wa St James Park hali ilikua ngumu kwelikweli kwa vijana wa Guardiola waliotangulia kufunga goli kupitia kwa Raheem Sterling. Vijana wa Newcastle waliamkaa kipindi chote cha pili nakuikosakosaa city huku wachezaji wa Man City wakiomba mpira uishe.

C. Palace 0 vs City 0

Hakika moja ya mechi iliyowalaza na viatu Man City ni hii. Wakiwa ugenini walikutana na moto wa kina Zaha katika dakika zote tisini kiasi walikaribia kupoteza mchezo baada ya C.Palace kukosa tuta katika dakika ya 93 ya mchezo. Ni kama bahati tuu City kupata point katika mchezo huu.

 Burnley 1 vs City 1

Burnley waliendelea kuonyesha wao ni kiboko ya vigogo EPL baada ya kuidhibiti City na kugawana point. Alianza Danilo kuipa uongozi City kama Burnley kuchomoa dakika ya 88 kupitia kwa Gudmundsson.  Mpaka dakika 90 zinakwisha mchezo ulibaki sare ya bao moja kwa moja.

Image result for manchester city vs chelsea 2018

City 1 Chelsea 0

Manchester City walifanikiwa kuizima kwa mara ya pili Chelsea katika ligi baada ya goli zuri kutoka kwa Bernardo Silva na kunyakua Point tatu muhimu kuelekea ubingwa. Pia game ya kwanza City alipata ushindi kama huo wa bao moja kwa bila, bao likifungwa na Kevin De Bruyne.

Image result for manchester city champions 2018

City 5 vs Liverpool 0

Leroy Sane na Gabriel Jesus kila mmoja akifunga goli mbili na Sergio Aguero akiweka moja yalitosha kuipa mkono liverpool iliyokua nusu baada ya Saído Mané kulimwa kadi nyekundu. Baada ya ushindi huo dhidi ya Liverpool, City walizidi kujuamini kuelekea mbio za ubingwa.

 

Totenham Hotspur 1 vs City 3

Hii ndio mechi ya mwisho iliyoipa ushindi Manchester City, lakini ilibidi wasubiri mpaka majirani zao Utd kupoteza  moja kwa sifuri mbele ya West Bromwich Albion.

Baada ya kipigo cha bao moja kwa sifuri kwa Manchester utd ni kama imejirudia msimu wa 2016 ambapo Leicester City alichukua ubingwa baada ya sare ya mabao mawili kwa mawili kati ya Chelsea na Totenham Hotspur.

Image result for manchester city champions 2018

Ilikua ikionekana mechi ngumu kwa City katika uwanja wa Wembley lakini sivyo, kwani Spurs walipotea wakiwa kwao na kukubalii kuhalalisha ubingwa wa City msimu huu. Magoli ya City yalifungwa na Gabriel Jesus, Ikar Gundogan na Raheem Sterling, huku Christian Eriksen akifunga bao pekee la Spurs

Sambaza....