Blog

Meneja: KMC waumini wa soka la vijana.

Sambaza....

Katika kuhitimisha story mbili tatu Ally Ramadhani “Kibampani” pia tulikutana na meneja wake Imani Mandu “Manucho” ambae hakusita kusifia na kukubali mpango mzuri wa klabu ya KMC katika soka la vijana.

Meneja wa mchezaji huyo ambae pia msomi wa masomo ya sheria anasema mpango wa klabu kama KMC ni mzuri na unamanufaa kwa nchi haswa katika kipindi hiki ambacho nchi yetu inachukua hatua katika kubadili mfumo wetu na kuelekea kwenye mpira wa kisasa.

Kevin Kijiri “Kevin Nash” akiwa na Ally Ramadhani “Oviedo”

Imani Mandu “Oviedo amefanikiwa kupata nafasi KMC  katika kikosi cha kwanza kwasababu klabu wanaamini katika soka la vijana na wana mipango mizuri kwa vijana cbipukizi kama yeye.

Tazama mfano mzuri ni yule Ally Msengi ambae kwasasa yupo nchini Africa Kusini anacheza soka la kulipwa lakini alipitia KMC hapa kabla ya kumruhusu kwenda huko.”

Abdul Hillal “Kijibwa” akiwa na Ally Ramadhani “Oviedo” wakiwa African Lyon B.

Ally Ramadhani mchezaji wa zamani wa African Lyon akiwa katika kikosi cha vijana (U-20) alijiunga na KMC baada ya kufanikiwa  kufuzu katika majaribio yaliyofanyika katika uwanja wa Bora-Kijitonyama chini ya Mwalimu mzoefu nchini Mbwana Makata. Wakati anakwenda kufanya majaribio hayo tayari alikua amemaliza mkataba na Klabu ya Changanyikeni Rangers.

Meneja pia alizungumzia sababu ya Ally Oviedo kudumu kwa muda mrefu na klabu ya KMC  huku akisema ni mipango endelevu ya klabu pamoja na maslahi mazuri kwa mteja wake.

Ally Msengi akiruks juu kupiga kichwa katika mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Coastal Union!

“Ni timu yenye mipango endelevu kwa vijana na waumini wa soka la vijana kama yeye, lakini pia ni  timu inatoa maslahi mazuri kwa wachezaji.” Imani “Manucho”.

Kwa upande wake Ally Ramadhani anaamini KMC haitoshuka daraja wao kama wachezaji watapambana mpaka hatua ya mwisho ya ligi. Oviedo anasema kwa Bongo hapa ni shabiki mkubwa wa mchezaji mwenzake wa KMC Cliff Buyoya “Mbappe” wakati kwa Ulaya anamkubali Renan Lodi mlinzia wa kushoto wa Athletico Madrid .

 

Sambaza....