Serie A

Milan ilivyomsubiri Masia kuwaokoa!

Sambaza....

Usiku wa mwishoni mwa wiki Ac Milan imefanikiwa kutwaa ubingwa wake wa 19 katika historia yake Series A. Halikuwa jambo jepesi kutwaa ubingwa uliokuwa unamilikiwa na wapinzani wao Inter Milan.

Ac Milan wana’ Rosseneri’ wamemaliza wakiwa na alama 86 huku ikiwaacha wapinzani wao wa karibu Inter Milan iliyomaliza na alama 84.
Milan na Inter timu kutoka jiji la Milan wote kwa sasa wanakuwa wametwaa escudetto 19 tangu ligi hiyo ya Serie A kuanzishwa mwaka 1898.

AC Milan mabingwa wa Seria A 2021/2022

Kwa upande wa Milan wametwaa ubingwa baada ya miaka 11 tangu watwae kwa mara ya mwisho 2011.

Ubingwa huu wa Ac Milan umekuwa wa kuvutia ukiangalia vijirekodi kadhaa vilivyoshabihiana na ubingwa wao wa mwaka 2011.

Kwanza ni uwepo wa mchezaji Zlatan Ibrahimovich mimi hupenda kumuita ‘Ibrahimagic’ nikiwa na maana ya ‘Mwanamazingaombwe’ kwa hapa pia ndiye Masia aliyerejea kuwakomboa Wanamilan.

Mabingwa wa Seria A msimu 2010/2011 AC Milan.

Alikuwepo kwenye ubingwa wa mara ya mwisho miaka 11 iliyopita akichangia mafanikio hayo kwa goli 14 katika michezo 28 aliyocheza.

Msimu huu pia amechangia magoli 8 katika mechi 22 alizocheza na hivyo tutakubaliana Ac Milan alikuwa anamsubiri Masia huyu kuja kuwaokoa tena.

Msimu wa mwaka 2011 Ac Milan alichukua ubingwa kutoka kwa mahasimu wao Inter Milan sawa kabisa na ubingwa wa msimu huu 2022 wamechukua toka kwa wapinzani wao hawa hawahawa.

Zlatan Ibrahimovic.

Rekodi nyingine inayoshahabihana ni mwaka 2011 wakati wa Inter Milan anachukua ubingwa wake wa 19 Milan alimaliza wa pili katika msimamo wa ligi. Kama ambavyo msimu huu 2021/22 Milan ikiwa inachukua ubingwa wa 19 Inter amekuwa wa pili.

Rekodi nyingine nzuri kwa Ac Milan ni golikipa wake Mike Maignan kuwa golikipa mwenye Clean sheet nyingi zaidi zilizopelekea kuwa mabingwa baada ya miaka 11.

Sawa na kile alichokifanya akiwa na Lille mwaka 2020/21 iliyopita akiwa na League 1 na kuwapa ubingwa ambao ulikuwa wa kwanza tangu timu imeanzishwa.

Mlinda mlango wa AC Milan.

Kitu ambacho amekirudia msimu 2021-2022 akiongoza kwa Clean sheet na hatimaye ya kuwapa ubingwa baada ya miaka 11.
Pamoja na timu za Italy kukaa na mchezaji kwa muda mrefu kwa upande wa Ac Milan hakuna mchezaji aliyekuwepo katika ubingwa wa msimu 2011.

Pia Ac Milan wamekuwa kama na bahati katika tarehe 23/May/ wamewahi kutwaa ubingwa mara 4 kwenye mashindano tofauti kwenye European Cup 1968 na 1990 pia Escudetto 2007 na pamoja ya sasa zote zilikuwa katika tarehe hiyo.

Hivyo tunaweza kusema Zlatan ‘Mwanamazingaombwe’ huyu ndiye Masia wa Ac Milan

Sambaza....