Serie A

Buffon: Nitacheza mpaka na wajukuu zao

Sambaza....

Mlinda mlango Nguli duniani Gigi Buffon ambae kwa sasa anawatumikia Vibibi vizee vya Turin Juventus baada ya mchezo wa jana dhidi ya AC Milan alitoa kali ya mwaka.

Baada ya mchezo wa nusu fainali ya kwanza kati ya AC Milan na Juventus ulioisha kwa sare ya bao moja kwa moja kumalizika Gigi aliomba jezi ya kinda wa AC Milan Daniel Maldin.

Gigi Buffon akiongea na waandishi wa habari baada ya mchezo kumalizika akiwa na jezi ya Daniel Maldini!

Alipulizwa na waandishi baada tukio lile Gigi Buffon alijibu “Kwenye mkusanyiko wangu nina jezi ya Chiesa na mwanae, nina jezi ya Thuram na mwanae, nina jezi ya Weah na mwanae na sasa nina jezi ya Maldin na mwanae. Sasa nasubiri wajukuu zao.”

Baada ya majibu hayo Gigi alionekana kucheka na waandishi huku akiwa ameiweka begani kwake jezi ya Daniel Maldini. Kwa sasa Buffon ana miaka 42 akiwa ameitizimia mapema January 28 mwaka huu.

 


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.