Blog

Mkataba wa Magori umeisha Simba

Sambaza....

Kumekuwa na taarifa za ndani kuwa Mtendaji mkuu wa Simba , Magori kuondoka Simba na kuna habari za mtendaji mpya kutoka nje ya nchi kuchukua nafasi yake.

Mwenyekiti wa klabu ya Simba amedai kuwa mkataba wa Magori umeisha lakini bado anaendelea kuhudumu ndani ya klabu hiyo.

Magori (Kulia) wakati wa mechi dhidi ya TP Mazembe, Robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika 2019.

“Ni kweli alikuwa na mkataba wa miezi 6 na mkataba wake umeisha kwa sasa. Ila bado anaendelea kuwa mtendaji wa Simba mpaka pale tutakapotangaza jambo jingine”- alidai mwenyekiti huyo wa Simba, Sued Kwambi.

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x