BlogEPL

Mmoja akamatwa, kwa maneno ya kibaguzi dhidi ya Beki wa Wigan

Sambaza kwa marafiki....

Kijana mmoja nchini Uingereza amejisalimisha mwenyewe Polisi mjini Blackpool baada ya kuandika maneno ya kibaguzi kwenye akaunti ya Twitter kuelekea kwa mlinzi wa Wigan Nathan Byrne.

Kijana huyo amejisalimisha wakati ambapo Polisi wakiwa katika uchunguzi kufuatia klabu ya Wigan kupeleka malalamiko baada ya mashabiki kadhaa kuandika maneno ya Kibaguzi kwa mlinzi huyo kufuatia sare ya mabao 2-2 na Bristol City katika mchezo wa ligi ya washindi England siku ya Jumamosi.

Kijana aliyejisalimisha Polisi ana umri wa miaka 20 na anatokea katika mji wa Sheffield na ni mwanafunzi katika Chuo cha Liverpool Hope na tayari amefunguliwa mashtaka licha ya kuachiwa huru kufuatia kitendo ambacho amekifanya huku mashabiki wengine wakiwa wanatafutwa.

Kufuatia tukio hilo chama cha soka England kimesema kuwa kunasikitishwa kwa vitendo vya kibaguzi vinavyoendelea licha ya juhudi kubwa wanazofanya kupunguza vitendo hivyo michezoni “Ni jambo la kusikitisha, la kukatisha tamaa na kutia hasira kusikia vitendo vya kibaguzi vinaendelea,”.

Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.