Blog

Morali na mafanikio ya wachezaji wa Simba ilichangia pia-Himid Mao

Sambaza kwa marafiki....

Tovuti ya kandanda ilipata nafasi ya kufanya mhojiano na Nahodha msaidizi wa kikosi cha timu ya Tanzania (Taifa Stars), Himid Mao Mkami, ambaye kwa sasa anacheza soka la kulipwa nchini Misri katika klabu ya Petrojet.

Ulikuwa wasaa mzuri kupata ushirikiano mzuri kutoka kwa kiungo huyu ambaye ameichezea Azam Fc pia hapo kabla. Katika mfumo wetu wa leo tutakuwekea maswali yetu na majibu yetu, unaweza pia endelea kufuatilia tovuti yetu kwa uchambuzi zaidi kuhusu mahojiano haya.

Himid Mao (wa pili kutoka kushoto) akiimba wimbo wa Taifa kabla ya mchezo wao wa mwishi dhidi ya Uganda.

Tanzania kwa mara ya pili baada ya miaka takribani 39 ilifuzu katika michuano ya mataifa ya Afrika baada ya kuichapa Uganda mabao 3-0. Kwa upande wa Himid tulipomuuliza mechi hiyo ilikuwa na maana gani kwake binafsi, kabla na baada hili ndio lilikuwa jibu lake:

“Ilibeba matumaini ya watu zaidi ya milioni 50 wa Tanzania na mimi nilikua mmoja ya wanaotakiwa kufanya timu ifuzu, kwahiyo ilikua na presha kubwa kwangu na wenzangu kwa ujumla”

Mashabiki wa Stars

Wachezaji wengi huwa wanakuwa na usongo wa kusubiria mechi fulani, fikiria hata sasa wachezaji wa Simba wanavyoisubiria Sevilla. Je Himid Mao yeye ashawahi kukosa usingizi akiwazia mechi fulani kuwa itakuwaje? Mechi ipi?

“Imeshatokea mara nyingi tu lakini kadiri ninavyokua na kucheza mechi nyingi nakua nazoea, ni mechi nyingi (ambazo zimemfsnya kuwazia ksbla ya mechi husika)” Himid Mao.

Tulijaribu kujua pia Nahodha Mbwana Samatta ni neno gani la motisha aliwaambia wachezaji kuhusu mechi ya Uganda alipokutana nao.

Samatta akiwashukuru mashabiki

“Daima Sam (Samata) ni muhamasishaji kwa wachezaji wote na sio kwa maneno tu hata mazoezini hadi kwenye mechi kwa vitendo, ila kubwa ilikua tunaongea ni lazima tufuzu tena ilikua kabla hata ya mechi ya Lesotho”

Kuhusu kuhuzunishwa na matokeo ya Stars mpaka ukajuta kuwa bora ungekuwa mchezaji wa Taifa jingine, Himid alituambia ni kweli amewahi huzunika lakini kamwe haikubadilisha itaifa wake.

“Nimeshawahi kuhuzunika sana pamoja na kulia kutokana na matokeo ya Taifa Stars lakini sijawahi kujutia kuwa Mtanzania au kuwa mchezaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania, naamini ipo siku Tanzania itakua kuja kubwa kwenye mpira” Mao

Wakati Taifa Stars inatafuta tiketi ya AFCON, klabu ya Simba ilikuwa katika hatua nzuri ya kutinga robo fainali ya Klabu Bingwa Afrika. Tulijaribu kujua pia kama Mafanikio ya klabu ya Simba yalikuwa yotote kabla ya mechi ya Uganda.

Wachezaji wa Simba wakishangilia mara baada ya kutonga Robo fainali ya klabu bingwa Afrika.

“Nadhani yalikua na maana kubwa sana kwao kama klabu na wachezaji wao, nawapongeza kwa hilo ila timu ya Taifa ni timu nyingine japo wachezaji wao walikuja na morali na kujiamini zaidi kutokea kwenye klabu yao, …hicho ndio kizuri.”

Kwa upande wa wapi angetamani kwenda kucheza, Himid alituambia ndoto anayo lakini vitu ambavyo anaangalia ni sehemu yenue ligi bora na sehemu ambayo inaweza kumpeleka atakako.

“Ndoto zipo na kwenye mpira. Ulipo ndio panamaana kubwa sana ya kukupeleka unapotaka kwa kufanya vizuri kwanza hapo. Kwa upande wa nchi, ni yeyote ile, ila nitaangalia pawe pana ushindani na ligi bora zaidi ya niliyopo kama nilivyofanya wakati nakuja hapa (Petrojet)”

Himid Mao Mkami, akiwa Petrojet Fc

Himid hakuwema wazi ni klabu ipi kwa Tanzania ambayo anatamani kuja kuichezea hapo baadae kama ikitokea

Tanzania imepangwa katika kundi C katika michuano ya AFCON 2019 inayofanyika nchini Misri. Utayari na mtazamo tofauti wa maahindano haya kwa kila mchezaji anayeitwa kujua umuhimu wake na kuchukulia kuwa ni mashindano na sio hatua ya kufuzu. Hiki ndicho tulichokipata kutoka kwa Himid.

“Ni mashindano haya sio qualification (kufuzu) inatakiwa approach(mtazamo) tofauti kujipanga kwetu na kuwa tayari ndio kutabeba matumaini yetu kama timu na taifa kwa ujumla, siwezi ahidi kitu” Himid alikazia zaidi.

Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.