Blog

Mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Czech afariki dunia kwa ajali.

Sambaza kwa marafiki....

Mshambuliaji wa kimataifa raia wa Czech Josef Sural amefariki dunia kufuatia ajali ya gari lililokuwa limewabeba wachezaji wa timu ya soka ya Aytemiz Alanyaspor kupata ajali wakati wakirudi nyumbani baada ya kumaliza mechi.

Sural ambaye ni mchezaji wa timu ya Taifa ya Czech amefariki wakati akipatiwa matibu hospitalini wakati ambapo yeye na wenzake sita waliokuwa wamepata ajali hiyo walipokimbizwa hospitalini kwa ajili ya kupatiwa huduma ya kwanza kutokana na ajali hiyo iliyotokea KM5 kusini mwa mji wa Alanya nchini Uturuki siku ya Jumapili.

Wachezaji saba wa Alanyaspor walikodisha bus dogo kurudi nyumbani baada ya mchezo wao dhidi ya Kayserispor uliomalizika kwa sare ya 1-1 siku ya Jumapili na ndipo wakapata ajali wakiwa njiani, huku wachezaji wengine pamoja na viongozi wa klabu wakirudi kutoka kwenye mchezo huo kwa kutumia Bus la timu.

Mwenyekiti wa klabu ya Aytemiz Alanyaspor, Hassan Cavusoglu amenukuliwa akisema kwamba dereva wa Bus lililopata ajali alipitiwa na usingizi wakati ambapo dereva wa pili akiwa amelala wakati ambapo ajali hiyo ilipotokea.

“Kutokana na taarifa nilizozipata kutoka kwa maofisa wa polisi, ni kwamba japokuwa kulikuwa na madereva wawili kwenye lile gari, lakini wote walikuwa wamelela, na ajali imetokea kwa kuwa wote walikuwa wamelala,” amesema.

Ameongeza kuwa wachezaji wengine sita ambao walikuwa kwenye gari lililopata ajali hali zao zinaendelea viruzi na hawana majeraha ya kutisha sana.

Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.