Mabingwa Afrika

Mwamuzi ’aliyewahi tuhumiwa’ ndiye kuongoza Simba ugenini

Sambaza kwa marafiki....

Janny Sikazwe ndiye mwamuzi wa kati aliyeteuliwa leo na CAF kuchezesha mechi ya mkondo wa pili kati ya TP Mazembe na Simba Sc, Sikazwe ambaye ni raia wa Zambia amechukua nafasi ya Mwamuzi kutoka Ethiopia baada ya mabadiliko ambayo shirikisho la kandanda Barani Afrika (CAF) ambayo imeyaita ya kiufundi.

Wasiwasi umeshatanda kwa upande wa klabu ya Simba juu ya mabadiliko haya, hadi kupelekea kuandikwa kwa barua ya malalamiko mara moja kwenda CAF kuhusu hili.

Katika pita pita za Kandanda.co.tz tumegundua kuwa mwamuzi huyu licha ya utata wa mabadiliko ya ghafla, lakini amewahi tuhumiwa kupokea rushwa mwaka jana na shirikisho hilo hadi kupelekewa kusimamishwa hadi uchunguzwi ufanywe.

Alipewa mashtaka hayo baada ya mchezo wa nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Esperance de Tunis ya Tunisa na Primiero Agosto ya Angola, ambapo Esperance ilishinda bao 4-2 nyumbani.

Ingawa amezungumza mara nyingi kuwa hakuchukua rushwa, lakini tuhuma hizi ni za kuziangalia pia kwa makini wakati mwamuzi huyu anaenda kusimamia mechi muhimu ya klabu ya Simba Sc.

Sikazwe amewahi kuchezesha pia mechi za kombe la Dunia mwaka 2018 na michuano ya dunia ya kwa vilabu mwaka 2016.

Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.