Ligi Kuu

Mwana wa mfalme asiyestahili ufalme!

Sambaza....

Alipokuja kwenye Ligi ya Tanzania nilisema moyoni mwangu ulisema waooo sasa ‘top quality player ‘ wameanza kuja nchini. Naheshimu “top quality player” tunao wengi lakini wanatofautiana kutoka kwa moja kwenda kwa mwingine.

Kiukweli Dube aliashiria kama yupo juu ya ligi yetu yaan maarifa yake hasa kwenye eneo la kufunga ni makubwa anafaa kuwepo kwenye ligi kubwa zaidi. 

Prince Dube akitambulishwa na mtendaji mkuu wa Azam Fc Abdulkarim Popat baada ya kujiunga na Azam Fc.

Alimaliza msimu akiwa na goli 14 akishika nafasi ya pili nyuma ya mzawa John Bocco na bado alizongwa na majeruhi ya mara kwa mara yaliyomfanya akose game nyingi za Ligi.

Meddie Kagere kwanini basi huyu ni mfalme seasons 4 alizocheza hapa ikiwemo hii ambayo ipo juu ya nusu kwa michezo 19 mwanaume kashaweka wavuni jumla ya magoli 65.
Kagere msimu wake wa kwanza goli 23 wa pili 22 na tatu 13 na huu 7 hadi sasa huku mwaka anafunga goli 22 akikosa kucheza michezo 8.

Meddie akiwa mazoezini.

Binafsi nilitaraji Dube anakwenda kurithi ufalme wa Meddie nikiamini yeye ni kijana zaidi na anaweza kuwepo kwenye ligi yetu kwa muda mrefu ujao.

Cha kushangaza na kusikitisha msimu huu upepo umeyumba sana kwa marejeo ya kumbukumbu zangu ana goli moja tu dhidi ya Namungo kwenye ushindi wa 1-2 kule Lindi

Nikafika mbali kumuangalia kiufundi nini tatizo? Nikagundua nafasi anapata lakini kupoteza umakini. Anachezeshwa na viungo bora wengi ndani ya timu yake lakini uwezo wake wa kufunga umeshuka sana kaondoka kwenye wastani wa mechi tatu bao moja au nafasi tatu goli moja.

Prince Dube “mwana wa mfalme”

Kaja kwenye nafasi 5 hakuna goli ,na mechi 19 goli moja hakika hawezi kurithi ufalme wa Meddie kwa maana ya mchezaji wa kigeni aliyefanya makubwa kwa muda mchache.

Ukimtizama katika mechi ya jana dhidi ya Polisi kwenye kombe la Azam federation amepata nafasi za kutosha lakini amekuwa na tatizo kubwa kwenye kumalizia kazi za kipunda zilizofanywa na wenzake.

Kama mtu mgeni wasifu humfahamu vyema mwanahuyu wa mfalme ukawa unasikia tu wasifu wake waweza kumuangalia bwana mdogo Ismail Azizi Kaddah ukadhani ndiye Mwana wa mfalme aliyeimbwa kote msimu uliopita, licha ya kuwa anafunga aina ya magoli yake yalikuwa na utofauti sana kwa kweli.

Rodgers Kola.

Mwana wa mfalme tuliza kichwa umrithi ufalme Meddie “ukidelay” huyo Rogers Kola atakuwa mrithi sahihi. Na zile ndoto za kufanya ligi ya ndani ni Platform ili utoke yawezekana ukawa wa humu humu na wengine wakatoka nyuma yako.

Sambaza....