Blog

Mwandishi aliyeibua rushwa michezoni, auwawa.

Sambaza....

Mwandishi wa habari za upelelezi nchini Ghana amepigwa risasi hadi kufa wakati akiendesha gari kwenda nyumbani kwake, baada ya mwanasiasa kuitisha adhabu dhidi yake.

Vyombo vya habari vya ndani vimeripoti kuwa watu wasiojulikana wakiwa katika pikipiki walimpiga risasi Ahmed Hussein-Suale mara tatu katika mji mkuu wa Accra.
Alikuwa ni miongoni mwa wahusika wa shirika binafsi la upelelezi Tiger Eye na alipepeleza rushwa katika ligi ya mpira wa miguu Ghana.

Taarifa hiyo ya uchunguzi kuhusu rushwa ilisababisha kufungiwa maisha kwa aliyekuwa kiongozi wa shirikisho la kandanda nchini Ghana.

Shirika la Utangazaji la Uingereza ‘BBC’ kupitia kipindi cha Afrikan Eye iliwahi kufanya makala kuhusu skendo hiyo ya rushwa mwaka 2018 baada ya kupata uchunguzi huo kwa ruhusa ya mwandishi machachari Anas Aremayaw Anas, ambaye anaiongoza Tiger Eye.

Baada ya BBC kurusha makala hiyo, mbunge wa Ghana Kennedy Agyapong alisambaza picha za mwandishi huyo Hussein-Suale na kutaka adhabu dhidi yake.

“Akija hapa mpige”, bwana Agyapong alisema kwenye video iliyochapishwa katika moja ya vyombo vya Ghana “chochote kitakacho tokea nitalipa.”

Kupitia mtandao wa kijamii bwana Anas amesema hawezi kunyamazishwa kimya kwa mauaji ya mwenzake.

Bwana Hussien-Suale alipigwa risasi mbili kifuani na moja shingoni majira ya saa 23:00 siku ya Jumatano usiku, taarifa zinasema.

Imeripotiwa kuwa mwili wake ulipelekwa katika hospitali ya polisi na atazikwa hivi karibuni.

Mwandishi huyo wa habari za upelelezi ameshirikiana na BBC katika taarifa kadhaa ikiwemo upelelezi wa uuzaji wa viungo vya watu kwa ajili ya shughuli za kichawi huko Malawi.

Matukio ya unyanyasaji waandishi wa habari ni ya nadra sana Ghana
Kwa mujibu wa IFJ mara ya mwisho mwandishi kuuawa nchini Ghana ni mwaka 2015.

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x