EPL

Mwili mmoja waopolewa, ajali ya ndege ya Emiliano Sala.

Sambaza kwa marafiki....

Mwili ulioonekana kwenye ndege iliyopata ajali siku chache zilizopita umeopolewa kutoka kwenye ndege iliyopata ajali iliyokuwa imembeba mchezaji mpya wa timu ya soka ya Cardiff City, Emiliano Sala na Rubani David Ibbotson.

Meli ya The Geo Ocean III iliyokuwa ibeba mwili huo iliwasili katika Bandari ya Portland mjini Dorset leo na tayari mwili huo umechukuliwa kwenda kufanyia vipimo vya vina saba na vingine kubaini mengine zaidi.

Familia za wale Emilliano na David zimehabarishwa kuhusu hilo na kwamba kila ambacho kitaendelea kujiri kitakuwa kikiharifiwa kwa familia husika.

Emiliano ambaye alisajiliwa kwa usajili uliovunja rekodi za Klabu ya Cardiff alipotea akiwa angani na ndege aina ya Pipre Malibu N264DB akitokea Ufaransa kuelekea Cardiff kujiunga na timu yake hiyo mpya.

Emilliano alisajiliwa kwa ada ya Uhamisho ya Paund Milioni 15 na ajali hiyo ilitokea siku mbili tu baada ya Cardiff kuthibitisha kufanya usajili huo, huku wakimtazamia kuwa pengine angejiunga nao lakini haikuwa hivyo.

Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.