Nantes' Argentinian forward Emiliano Sala (R) celebrates with his teammates after scoring a penalty during the French L1 football match between Nantes and Angers at Beaujoire Stadium in Nantes, western France, on December 17, 2017. (Photo by JEAN-SEBASTIEN EVRARD / AFP)
EPL

Polisi wathibitisha kifo cha Emiliano Sala.

Sambaza kwa marafiki....

Mwili ulioopolewa kutoka kwenye ndege umetambuliwa kuwa ni mshambuliaji wa Cardiff City Emiliano Sala, kama taarifa zilivyothibitishwa na kituo kikuu cha Polisi mjini Dorset.

Mwili huo hapo awali ulitambuliwa kuwepo kwenye ndege siku ya Jumatano na juhudi za kuutoa zilizaa matunda jana Alhamis na baada ya hapo ukapelekekwa kwenye uchunguzi kufahamu kwa kina ni mwili wa nani.

Taarifa ya polisi leo asubuhi imesema kuwa mwili huo ni mshambuliaji Emiliano Sala ambaye yeye pamoja na Rubani David Ibbotson walipata ajali Januari 21 wakati wakitokea mjini Nantes Ufaransa kuelekea Cardiff Uingereza.

“Mwili uliletwa hapa Alhamis February 7, 2019, na umetambuliwa kuwa ni mwili wa mchezaji wa mpira Emiliani Sala, tayari familia ya Sala na ya rubani David imetaarifiwa kuhusiana na taarifa hizi, na tutaendelea kuwa na pamoja katika kipindi hiki kigumu,” Taarifa ya Polisi imeeleza.

Mshambuliaji huyo raia wa Argentina alijiunga na Cardiff City ya ligi kuu England akitokea Klabu ya Nantes ya Ufaransa kwa ada ya Paund Milioni 15, lakini hakufanikiwa kucheza hata mchezo mmoja kwani wakati akisafiri kujiunga na klabu yake mpya ndipo ajali ilipotokea.

Mpaka anaondoka nchini Ufaransa alikuwa tayari ameshafunga mabao 12 katika michezo 19 ya ligi kuu, huku akitoa msaada wa mabao mawili kwa timu yake ya Nantes.

Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.