Sportpesa

Sevilla: Tuna shauku ya kucheza na Simba!

Sambaza kwa marafiki....

Homa ya mchezo wa kirafiki wa Kimataifa kati ya Simba sc ya Tanzania na Sevilla fc ya Hispania imepamba moto. Mchezo huo utapigwa katika dimba la uwanja wa Taifa siku ya tarehe 23 May mwaka huu.

Mlinda mlango wa Sevilla fc inayoshiriki Laliga wakiwa nafasi ya 6 ameshindwa kuficha hisia zake na kuonyesha ana hamu kiasi gani ya kukipiga katika dimba la Taifa “Kwa Mkapa” jijini Dar es salaam.

Kipa wa Sevilla fc Tomas Vaclik amesema ” Tunakuja Tanzania tukiwa ndio timu ya kwanza kutoka Laliga (Spain) kuja kucheza Tanzania. Tuna shauku kubwa, huku tukiwa na matarajio makubwa ya kufika huko. Tunakuja huko muda si mrefu.”

Ikumbukwe Sevilla sc mabingwa mara 5 wa Europa League wanakuja kucheza Tanzania kwa mara ya kwanza wakiletwa kwa udhamini wa Sportpesa walio na uhusiano mzuri na uongozi wa Laliga nchini Hispania.

Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.