Mabingwa Afrika

Simba kaishangilieni Yanga leo- Manara

Sambaza kwa marafiki....

Leo vilabu vyetu vinne vinaanza kutuwakilisha katika michuano ya soka barani Africa kwenye michuano ya vilabu.

Tanzania inawakilishwa na vilabu vinne mwaka huu. Vilabu hivo ni Simba na Yanga vitakavyocheza katika michuano ya klabu bingwa barani Afrika.

KMC na Azam FC watatuwakilisha katika michuano ya kombe la shirikisho barani Afriƙa. Nafasi hizi nne zimepatikana baada ya kupata alama nyingi kutokana na kufanya vizuri katika michuano ya klabu barani Afrika.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, afisa habari wa Simba, Haji Manara amewaomba mashabiki wa Simba kwenda kuishangilia Yanga leo.

“Najua msimu jana walishangalia wapinzani , lakini sisi tusiwafanyie hivo. Hili ni jambo la kitaifa, ni jambo ambalo linaweza kutuongezea alama za kupata ongezeko la timu kwenye michuano ya vilabu barani Afrika”- aliandika Haji Manara

Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.