Blog

Simba kutumia kadi za Equity Bank

Sambaza kwa marafiki....

Klabu ya Simba imeingia mkataba wa miaka saba na Benki ya Equity kwa ajili ya kutengeneza kadi mpya za wanchama amabazo zitakuwa na huduma zote za kibenki.

Kadi hizo zitakuwa za aina mbili ambazo ni za Wanachama na za Mashabiki (Fans Card) ambazo zitaitwa Simba Card.

Kwa wale wanachama ambao wana kadi za zamani watabadilishiwa na kupewa mpya wakati ambao hawana watalipia shilingi 10,000 kama zile za mashabiki ambapo kila mwezi watalipia shilingi 1000.

Mtendaji mkuu wa klabu ya Simba, Crescentius Magori amesema hakutahitajika kuwa na pesa ya kianzio katika akaunti wala makato ya mwisho wa mwezi.

Tafadhali tumia viungo rasmi kusambaza habari zetu. Facebook, Twitter au Barua Pepe. Kama utataka kutumia habari zetu tuandikie kupitia habari@kandanda.co.tz